Posted Alhamisi,Juni26 2014 saa 14:7 PM
Kwa ufupi
Nigeria imefuzu, lakini katika mechi yao ya jana
ilichapwa 3-2 na Argentina, ambapo mabao ya Argentina yalifungwa na
Lionel Messi dakika ya 3 na 45 na Marcos Rojo (50) huku mabao ya Nigeria
yakifungwa na Ahmed Musa (4, 46).
Rio de Janeiro, Brazil. Timu za taifa za Nigeria, Ufaransa na
Uswisi zimetinga hatua ya 16 bora ya Fainali za Kombe la Dunia 2014
baada ya kushinda katika mechi zao za mwisho za hatua ya makundi jana.
Nigeria imefuzu, lakini katika mechi yao ya jana
ilichapwa 3-2 na Argentina, ambapo mabao ya Argentina yalifungwa na
Lionel Messi dakika ya 3 na 45 na Marcos Rojo (50) huku mabao ya Nigeria
yakifungwa na Ahmed Musa (4, 46).
Messi amecheza mechi tatu amefunga mabao manne na
katika mechi zote tatu amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi. Tayari
Argentina imefuzu pia.
Vile vile, kocha Stephen Keshi wa Nigeria amekuwa kocha wa kwanza wa Kiafrika kuifikisha timu ya Afrika katika hatua ya 16 bora.
Katika mechi nyingine iliyochezwa jana, Bosnia
& Herzegovina iliichapa Iran 3-1. Mabao ya Bosnia yalifungwa na Edin
Dzeko (23), Miralem Pjanic (56) na Avdija Vrsajevic (80) wakati bao la
Iran lilifungwa na Reza Ghoochannejhad dakika ya 79.
Ufaransa yenyewe imefuzu baada ya kutoka sare ya
0-0 na Ecuador Wakati Uswisi imefuzu baada ya jana kuichapa Honduras
mabao 3-0. Mabao yote matatu ya Uswisi yalifungwa na Xherdan Shaqiri (6,
31 na 70).
Timu ambazo zimeishafuzu mpaka sasa ni Brazil,
Chile, Colombia, Uruguay, Uholanzi, Mexico, Costa Rica, Ugiriki,
Argentina, Nigeria, Ufaransa na Uswisi.
Post a Comment