Baada ya vuta ni kuvute huku ikitishiwa kulimwa adhabu na
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), klabu Yanga imekubali matokeo na
kumalizana na wachezaji wake wa zamani, Stephano Mwasika na Shadrack
Nsajigwa ‘Fusso’ waliokuwa wakiidai klabu hiyo zaidi ya Sh15 Milioni.
Wachezaji hao walikuwa wanaidai Yanga fedha hizo
kutokana na malimbikizo ya ada ya usajili, ambapo uongozi wa klabu hiyo
ulikuwa ukiwapiga danadana kuwalipa wakati walipokuwa waikiitumikia.
Kutokana na hali hiyo wachezaji hao baada ya
kuachwa na klabu hiyo katika usajili wake wa msimu huu waliamua
kuishtaki Yanga ili iweze kuishinikiza na kuwalipa haki zao.
Nsajigwa, alikuwa akiidai Yanga kiasi cha Sh 9
milioni wakati Mwasika ambaye sasa anaitumika Ruvu Shooting alikuwa
akiidai Yanga Sh 6.5 milioni.
Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako ameliambia gazeti hili jana kuwa wamemalizana na wachezaji hao siku tatu zilizopita.
Alisema Yanga haikuwa na nia ya kuwadhulumu
wachezaji hao isipokuwa malipo yao yalichelewa kutokana na kuwepo kwa
sababu mbalimbali za kiutawala.
“Tumemalizana nao, lakini ni vema ukawauliza na wenyewe kwa uhakika zaidi,” alisema Mwaluko.
Hata hivyo Nsajigwa alipouliwa alikubali kuwa
tayari wamemalizana na klabu hiyo tangu siku ya Jumatatu na sasa hana
kitu chochote anachoidai klabu hiyo.
Post a Comment