Ujumbe wa Tanzania ukiangalia ramani ya Singapore inayoonyesha ujenzi wa
miundombinu na makazi mbalimbali ya watu. Picha na Neville Meena.
Meenaaktaba.
Mnunuzi wa nyumba Singapore analipa aina moja ya kodi.
Singapore. Mambo haya matatu ni
kikwazo cha kukua kwa sekta ya nyumba nchini na tunapozungumzia sekta
hii hatuwezi kuweka kando Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ambalo
limeanza kujenga na kuwauzia Watanzania nyumba bora za kuishi.
Mambo haya mosi, ni riba kubwa ya mikopo ya
nyumba ya asilimia 18 inayowekwa na benki, pili ni kodi nyingi ambazo
zinatozwa katika vifaa vya ujenzi na tatu ni bei kubwa ya ardhi kwa
ajili ya ujenzi wa nyumba hasa maeneo ya mijini.
Nchini Singapore baadhi ya wabunge walifanya
ziara kujifunza jinsi nchi hiyo ilivyowekeza na kupata mafanikio katika
sekta ya makazi. Somo la kujifunza asilimia 82 ya watu milioni 5.3
nchini humo wanaishi katika nyumba zao.
Asilimia 18 iliyobaki sawa na watu 954,000 tu
wanaishi katika nyumba zilizojengwa na sekta binafsi na wengine kati ya
hao wanamiliki nyumba zao wenyewe.
Dalili za umahiri wa kuendeleza makazi inaonekana
tu unapoingia eneo la kukagulia hatia za kusafiria katika Uwanja wa
Ndege wa Changi, kwani mbele kuna tangazo kubwa linalonadi utaalamu huo
katika nchi hiyo ya Mashariki mwa Bara la Asia.
Majengo na miundombinu mingine katika nchi hiyo
ndogo yenye ukubwa wa kilometa za mraba 700, yamepangiliwa kwa ustadi
wa hali ya juu.
Wananchi hawajengi nyumba hizo wenyewe, bali ni
kazi ya Serikali, ambayo licha ya kwamba inaendelea kukusanya fedha za
mauzo mwaka hadi mwaka, imeweka utaratibu wa kusimamia kwa maana ya
matunzo, matengenezo na kukusanya kodi ya majengo na ardhi.
Mpango wa matumizi ya ardhi ulioandaliwa 1971 na kuanza kutekelezwa miaka 16 baadaye, 1987.
Matumizi ya ardhi yanajumuisha barabara, reli,
bandari, viwanja vya michezo, maduka, maeneo ya ukanda wa kijani,
viwanda na sehemu nyingine nchini Singapore.
Serikali ya Singapore ilitwaa ardhi karibu yote
kwa sheria ya Bunge ya 1966 na kuiwekea malengo ambayo yameleta manufaa
makubwa.
Shughuli za ujenzi na uendelezaji wa makazi zinafanywa na Kampuni ya Surbana inayomilikiwa na Serikali.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Surbana, Profesa Louis Tay anasema
Surbana hawanunui ardhi bali hupewa rasilimali hiyo kutoka katika Benki
ya Ardhi ya Serikali na kutekeleza mradi unaohitajika.
Katika mchakato wa ununuzi wa nyumba, benki za
Singapore zinatoa mikopo ya muda mrefu kati ya miaka 15 na 20, kivutio
kikubwa katika mikopo hiyo ni riba ambayo ni kati ya asilimia 2 na 3 tu,
viwango ambavyo ukizidisha mara sita ndio unafikia viwango vya
Tanzania.
Kwa upande wa kodi, uongozi wa Halmashauri ya Mji
wa Pwani ya Mashariki nchini Singapore, uliuambia ujumbe wa Tanzania
kwamba mnunuzi wa nyumba hulipa kodi ya aina moja tu na kwa kuwa nyumba
hizo ziko kwenye ghorofa moja, kodi husika hugawanywa kwa idadi ya
wanunuzi hao, hivyo ina unafuu mkubwa.
Tanzania
Tukirejea Tanzania wapangaji wa NHC na waliouziwa
nyumba, idadi yao ni sawa na asilimia 0.2 tu ya Watanzania wote na hii
inamaanisha kwamba watu wanaoishi katika nyumba hizo hawafiki hata
100,000.
Hivi sasa NHC wana wapangaji takriban 17,000 na
nyumba ambazo zimeuzwa kwa watu mbalimbali tangu 1961 ni 8,883, kati ya
hizo 5,383 ziliuzwa tangu lilipoanzishwa na mwaka 2010 zaidi ya nyumba
500 zimeuzwa kati ya mwaka 2011 na sasa.
Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Ardhi 2012,
ulibainisha kuwa wapangaji wa nyumba za NHC wako katika makundi matatu
kwa kuzingatia idadi ya wanafamilia; asilimia 43.3 ya nyumba hizo
zilikuwa na watu kati ya wanne na watano, asilimia 32.5 watu kati ya
mmoja na watatu na asilimia 20 zilikuwa na idadi ya watu sita na
kuendelea.
Hii inamaanisha kwamba zaidi ya asilimia 99 ya
Watanzania wanaishi ama katika nyumba za kupanga zilizojengwa na watu
binafsi, nyumba za Serikali au nyumba zao wenyewe.
Licha ya kwamba nchini Tanzania watu hutumia
nguvu zao kujenga, Taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) inaonyesha kuwa nchi inakabiliwa na upungufu wa nyumba
milioni 3, huku kukiwa na mahitaji mapya ya nyumba 200,000 kila mwaka.
Kwa upande wa ardhi, Tanzania hakuna mpango
kamili wa matumizi ya ardhi uliopitishwa na mamlaka rasmi. Hili ndilo
chimbuko la la migogoro mingi ambayo imesababisha baadhi ya watu
kupoteza maisha.
Baadhi ya wabunge ambao walikuwa nchini Singapore
katika ziara ya mafunzo kuhusu uendelezaji wa makazi, wanasema hasara
ya kuwa na ardhi isiyopimwa ni kukosa mapato kutokana na kodi.
Mbunge wa Kawe, Halima Mdee anasema hali hiyo pia ni kichocheo cha migogoro ya ardhi.Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Goodlucky
Ole Medeye anasema: “Tatizo kubwa ni fedha, uwezo wa kupima ardhi tunao
na tunaweza kufanya hivyo katika muda wa miaka mitano tukawa tumemaliza
nchi nzima endapo fedha zitapatikana.”
Kodi ya makazi
Wengine wanalalamikia ukubwa wa gharama za nyumba za NHC ambao unachangiwa na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Andrew
Chenge akizungumzia suala hilo anasema: “Katika nchi za Kusini mwa
Jangwa la Sahara, ni Tanzania pekee ambayo inatoza kodi kwenye makazi,
hili ni jambo la ajabu kabisa, aliyeishauri Serikali kuhusu suala hili
aliwapotosha.
Post a Comment