0
Dar es Salaam. Simba imeinyuka KMKM kwa mabao 2-1 katika mchezo wa kirafiki uliofanyika jana Uwanja wa Taifa. Simba ilipata mabao yake kupitia Said Ndemla na Giribert Kaze huku Idd Kambi akifunga bao pekee la KMKM.
Simba ilipata bao la kwanza katika dakika 35, kupitia Ndemla akimalizia vizuri pasi ya Issa Rashid. Kaze alifunga bao la pili kupitiawa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni.
KMKM walipata bao la kufutiua machozi kupitia kwa Kambi katika dakika 54. Katika hatua nyingine kocha wa Simba, Abdallah Kibadeni amewataka wachezaji wake kujituma kwa kuwa hakuna yeyote mwenye uhakika na namba katika kikosi cha kwanza.
Akizungumza na Mwananchi jana Kibaden alisema wote wanapaswa kupigania namba
isipokuwa wale wa kigeni pamoja na Henry Joseph, Nasoro Masuod (Cholro) pamoja na
Amri Kiemba.
Alisema mbali ya wachezaji hao, wengine waliobakia watakiwa wakipigania nafasi tatu
zilizobakia katika kikosi chake cha kwanza ambacho kitakuwa kikiongoza timu hiyo kwenye harakati zake za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu.
“Sitompanga mtu kwa sababu tu ni rafiki yangu, ila atakaye pata nafasi katika kikosi cha kwanza ni yule atakaye onyesha kiwango cha juu.
“Hadi sasa naweza kusema kuwa wachezaji wenye uhakika katika kiosi changu cha kwanza ni nane ambao ni Abel Dhaira, Joseph Owino, Hamis Tambwe, Gilbert Kaze, Amri Kiemba, Henry Joseph, Issa Rashid (baba ubaya) na Nassoro Masuod (Cholro).
“Wengine waliobakia wanatakiwa kupigania nafasi tatu zilizobakia,” alisema Kibadeni.
Nyota kama, Ramadhan Chombo (Redondo), Abdurahim Humoud, Shamte Ally kwa pamoja watatakiwa kupigana kwa nguvu ili waweze kupata nafasi za kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Simba ambacho hivi sasa kipo nafasi ya tano kwenye msimamo wa Ligi Kuu.

Post a Comment

 
Top