Dar es Salaam. Mjumbe wa kamati ya utendaji Shirikisho la Soka
Tanzania (TFF), Samweli Nyala jana amekata rufaa kupinga kuenguliwa
kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi.
Nyala ambaye anawania ujumbe wa mkutano mkuu
kupitia Kanda ya ziwa, Mwanza na Mara ameenguliwa kwenye kinyang’anyiro
hicho cha TFF kwa kile kilichoelezwa kuwa hakujaza kwa ukamilifu fomu za
maombi ya TFF na kuonyesha malengo yake.
Hata hivyo, Nyala alisema ameamua kukata rufaa kwa vile anaamini sifa zote anazo kwa
mujibu wa ibara ya 29 za katiba ya uchaguzi wa TFF na kanuni ya 1-7 ya uchaguzi ametimiza vigezo vyote.
“Kama elimu angalau kidato cha nne mimi ninayo, kama umri kuanzia miaka 18 mimi
nimepita kama ni suala la uzoefu wa miaka mitano ninao, hiyo fomu wanaosema sijajaza
kikamilifu ni fomu ipi? mimi sijaona.” alisema.
Post a Comment