Cape town, Afrika Kusini. Afrika leo itashuhudia makundi saba
yaliyosalia yakipata wawakilishi wao kwenye kufuzu kwa hatua ya mwisho
ya kusaka kucheza Kombe la
Dunia 2014.
Kati ya timu 10 zinazotakiwa kucheza hatua ya
mtoano ili kupata timu tano zitazokwenda Brazil mwakani ni Algeria,
Misri na Ivory Coast zenyewe zilikata tiketi hiyo tangu Juni.
Cameroon, Ghana, Nigeria, Senegal na Tunisia wanahitaji kupata sare nyumbani ili
kujihakikishia nafasi, lakini wapinzani wao wanaweza kuwashangaza kama watashinda
mechi za ugenini.
Ethiopia ni lazima waifunge Jamhuri Afrika Kati ili kujihakikishia nafasi hiyo kutoka kwa
Afrika Kusini ambao watakuwa nyumbani kuwavaa
Botswana. Congo watawavaa Niger, na Burkina Faso dhidi ya Gabon, timu
hizo zote bado zina nafasi ya kusonga mbele.
Vinara 10 wa makundi wataingia kwenye ratiba rasmi
ni Sept . 18 kwa ajili ya mechi mbili za mtoano zitakazofanyika Oktoba
na Novembaer, na kupata timu tano zitakazokwenda Brazil.
Ghana watakuwa na kibarua kizito mbele ya Zambia mshindi katika mchezo huo atakata
tiketi kwa hatua ya pili. Senegal, wanamatumaini
ya kufuzu kwa Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu walipocheza
fainali hizo mwaka 2002, watawakaribisha Uganda jijini Marrakech,
Morocco leo kutokana na kufungiwa kucheza uwanja wao wa nyumbani.
Senegal inaongoza kwa pointi moja mbele ya Uganda katika Kundi J.
Nigeria ipo mbele kwa pointi mbili kwa wapinzani
wake Malawi katika Kundi F kabla ya mchezo huo wa leo huko Calabar, huku
mechi hiyo ikifunikwa na jinamizi la ubaguzi wa rangi.
Kocha wa Malawi, Tom Saintfiet amelalamika kwa Fifa kuwa kocha wa Nigeria, Stephen
Keshi alimwita ”mtanashati ambaye anatakiwa kurudi
Ubelgiji.” Samuel Eto’o, ambaye amejiunga na Chelsea akitokea Anzhi
Makhachkala, ataiongoza Cameroon kuwavaa Libya jijini Yaounde kesho.
Cameroon imeiacha Libya kwa pointi moja katika Kundi I baada ya kipigo cha mabao 2-0
kutoka kwa Togo pale Juni kubadilika na kuwa ushindi wa mabao 3-0 kutokana na Togo
kuchezesha wachezaji waliofungiwaaliyefungiwa.
Tunisia inapewa nafasi ya kuongoza Kundi B kutokana na kuwaacha wapinzani wao Cape
Verde kwa pointi mbili kabla ya mchezo wa leo jijini Tunis, mchezo ambao mashabiki
wameruhusiwa kuangalia mechi hiyo pamoja na kuwepo matatizo ya kiusalama
Ethiopia, ambaoye imeiacha Afrika Kusini kwa pointi mbili na tatu zaidi ya Botswana,
wataondoka wakiwa vinara wa Kundi A, kamawataifunga Jamhuri Afrika Kati
huko Brazzaville.
Ethiopia watatoka sare watafungua njia kwa Afrika Kusini kufuzu kama watawafunga
Botswana kwenye mchezo wa mwisho utaochezwa Durban. Congo
inaongoza Kundi E, lakini wanafutiwa kwa karibu na Burkina Faso
wakitofautiana kwa pointi moja.
Congo watafuzu kama wataifunga Niger, huku Burkina Faso wakiwavaa Gabon.
Post a Comment