Kocha Stewart Hall
YANGA ikiteleza kidogo tu itapigwa bao la maana na Azam. Klabu
tajiri ya Azam FC imeanza kumnyemelea kwa siri kiraka Mnyarwanda, Mbuyu
Twite.
Mbio za Azam kumwania Twite zilionekana mara baada
ya kumalizika kwa mechi ya Ngao ya Jamii baina ya timu hizo kwenye
Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Kocha Mkuu wa Azam FC, Mwingereza Stewart Hall
aliachana na wachezaji wote wa Yanga akaenda moja kwa moja alipokuwa,
Mbuyu na Mrundi Didier Kavumbagu.
Alimsalimia Kavumbagu na baadaye akaenda kwa Mbuyu na kuzungumza naye kwa muda mrefu.
Ingawa Mbuyu hakutaka kuzungumza lolote kuhusiana
na hali hiyo, lakini mtu wake wa karibu alisema Azam inamtaka mchezaji
huyo na Hall alikuwa anamuuliza mkataba wake unamalizika lini na
alipomjibu bado mwaka mmoja akaahidi kumpigia simu baadaye wazungumze
kwa kina.
Mbuyu alisema: “Alikuwa ananipongeza kwa mchezo na mambo mengine (huku akicheka).”
Mwanaspoti ambayo lilikuwa
pembeni likishuhudia kila kilichokuwa kinaendelea, lilimnasa Stewart
akashtuka na kusema: “Nilienda kumpongeza tu sawa na nilipofanya kwa
wachezaji wengine wa Yanga.”
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Abdallah
Bin Kleb alisema: “Kama kuna timu inamwania mchezaji wetu yeyote si
halali kwa sasa kwa sababu wachezaji wetu wote wana mikataba zaidi ya
miezi sita.”
Post a Comment