Habari kutoka mkoani Gedo ulio upande wa kusini magharibi mwa Somalia
zinaarifu kuwa ndege za kivita za Jeshi la Kenya limefanya mashambulio
katika kijiji kilio chini ya mji wa Beled Haawo.
Mapema
leo nyakati ya Adhuhuri Ndege ya kijeshi kutoka Kenya kilidondosha
mabomu kadhaa kwenye kijiji cha Gaddoon Dawe iliyo karibu sana na mpaka
wa kizushi kati ya Kenya na Somalia.
Duru
ziliarifu kuwa mifugo kadhaa yakiwemo Mbuzi na Ngamia zimeathiriwa na
mashambulio hayo ingawa hakuna maelezo zaidi kuhusiana na hasara rasmi
iliyopatikana kutokana na Ndege za Kenya kufanya mashambulio mapema leo.
Ni
shambulio la kwanza kufanywa na Kenya katika Ardhi ya Somalia tangu
kufanyika opresheni iliyosababisha hasara kubwa katika mji wa Garissa na
ambapo ilifanywa na Mujahidina wa Al-Shabab Al Khamisi iliyopita.
Post a Comment