Kuna maelezo zaidi yaliopatikana kuhusiana na shambulio lililofanyika
jana usiku katika mji wa Bosaso makao makuu ya mkoa wa Kaskazini
Mashariki mwa Somalia.
Mashambulio
hayo yaliokuwa ya kufuatana yalilenga eneo ambalo ulinzi wake
uliimarishwa vilivyo,shambulio la kwanza iliyofanyika nje ya lango kuu
la Ikulu ya Rais waliuliwa Maaskari wawili wa Utawala wa Puntland.
Shambulio
lingine lililofanyika katika mtaa wa New Bosaso imesababisha kujeruhiwa
vibaya mkuu wa Wilaya wa Armo katika utawala wa "Puntland".
Duru
za kuaminika zilieleza kuwa Mohamed Shire ambae alikuwa mkuu wa Wilaya
wa Armo amepata majeraha mabaya huko maaskari wake wawili wakiuawa.
Mashambulio
yalioitikisa mji wa Bosaso jana usiku ilisikika maeneo mengi ya mitaa
ya mji huo ambao walimwagwa wanamgambo wanaojulikana PIS ambapo ni
maalum kwa mapambano dhidi ya kile kinchoitwa Ugaidi.
Vikosi
vya Mujahidina wa Milima ya Golis wamefanya mashambulio kadhaa kwenye
maeneo maalum ya mji wa Bosaso ingawa mashambulio ya jana usiku hakuna
aliyedai kuhusika.
Post a Comment