Mazungumzo yanarejelewa tena hii leo kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran kwenye mji wa Lausanne
Mazungumzo
yanarejelewa tena hii leo kuhusu mpango wa nuklia wa Iran kwenye mji wa
Lausanne nchini Uswisi zikiwa zimesalia saa chache kabla ya kumalizika
kwa muda wa kuafikiwa makubaliano.
Mataifa sita yenye nguvu zaidi
duniani yanakaribia kuafikia makubaliano na Iran. Hatua zimepigwa kuhusu
njia za kuzuia na kufuatilia shughuli za kinuklia za Iran.Mwandishi wa BBC mjini Lausanne anasema kuwa tofauti kubwa bado zimesalia kwenye masuala kadha ikiwemo kuhusu ni njia ipi ya haraka vikwazo dhidi ya Iran vitaondolewa.
Iran inashikilia kukutu kuwa mradi wake wa Nyuklia ni wa kuzalisha umeme lakini mataifa ya Magharibi yanapinga yakihofia kuwa huenda Iran inapanga kutengeza silaha zenye nguvu za kitonaradi.
Mataifa hayo ya magharibi yanalenga kudumaza uwezo wa Iran wa kutengeza Silaha zenye nguvu za kitonaradi kwa zaidi ya mwaka mmoja ili wawaondolee vikwazo vya kiuchumi.
Marekani, Uingereza ,Ufaransa , Uchina, Urusi na Ujerumani na waziri wa Iran Mohammad Javad Zarif wanaendelea na mkutano huu huku makataa waliojiwekea wenyewe ikikaribia kukamilika.
Post a Comment