0
Maofisa wa Polisi nchini Pakistan wametangaza rasmi kuwa wakili aliyekuwa akimtetea Dakatari aliyefanya ujasusi sehemu aliyokuwa akiishi Sheikh Usama Bin Laden Amiri wa zamani wa Kundi la Al Qaida.



Habari kutoka nchini Pakistan zinathibitisha kuwa watu waliokuwa wamejihami na silaha walimpiga risasi Samiullah Afridi wakati alipokuwa akitoka nyumba kwake iliyoko mji wa Peshewar iliyo mji mkuu wa 3 nchini Pakistan.




Wakili huyo aliyeuawa alikuwa akifanya juhudi kubwa ya kuwaelezea kwa Majaji wakuu wa Pakistaan kuwa Daktari aliyehusika kumfanyia ujasusi Sheikh Usama Bin Laden hana dhambi yeyote,Daktari huyo alimfanyia ujasusi Shekhe kwa Makachero wa Marakeni hadi alipokutana na Mola wake mwaka 2011.



Makundi mawili ya Kiislaam yalioko nchini Pakistan yamedai kuhusika kifo cha Wakili huyo aliyekuwa mtetezi wa Daktari aliyehusika kumwua Sheikh Usama Bin Laden.

Post a Comment

 
Top