0
Wakati kukiwa na hali mbaya ya usalama nchini Kenya viongozi wa mikoa mbalimbali nchini humo hukimbia kutoka katika makao yao na kwenda mafichoni baada ya kushuhudiwa mashambulio ya mara kwa mara yaliomwaga damu.


Baraza la mji wa Mandeera wamethibitisha kuwa viongozi wa utawala wa mji huo nyakati za jioni huenda kujificha kwenye baadhi ya vijiji vilio nje ya mji wa Mandera kutokana na khofu ya mashambulio kutoka kwa Mujahidina wa Al-Shabab.




Mmoja wa viongozi wa Baraza la mji wa Mandera ameliambia Idhaa ya Kisomali ya BBC kuwa kutokana na hali mbaya ya usalama uliopo mkoa wa Kaskazini Mashariki mwa Kenya imesababisha viongozi wa mji wa Mandera kuhama kutoka katika majumba yao na kwenda mafichoni.



Amethibitisha kuwa Maofisa wa Polisi na yale ya kijeshi wanawaogopa vikosi vya Harakat Al-Shabab Al Mujahideen huko akitoa mfano kuwa wakaazi wa eneo la Fino walitoa taarifa kwa wanajeshi wa kuwepo kwa wapiganaji 23 katika eneo lao lakini Wanajeshi hao walikataa kupigana nao.
http://qaadisiya.net/maqal/wareysi%20mandheera.mp3

Post a Comment

 
Top