0


Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imetangaza kuwa imefunga kwa muda maalum kwa ofisi zake za Ubalozi zilizopo katika Ardhi ya Haramayn unaojulikana Saudia Arabia.



Shirika la Fox News linalowanukuu baadhi ya maofisa wa Kimarekani imetangaza kuwa taarifa walioipata majasusi wa Marekani imesababisha kufungwa kwa kazi zote za Kidiplomasia iliyokuwa ikifanywa na Ubalozi huo wa USA.




Wafanyakazi wote wa Ubalozi huo waliopo katika miji ya Jidah na Riyadh wameamrishwa kutofanya pilika wowote na kuwa makini na mashambulio yanayotarajiwa kutoka kwa wapiganaji wa Kiislaam.



Marekani imeonyesha wasiwasi wake kuhusiana na wapiganaji wa Kijihadi wanaopambana katika nchi za Iraq na Syria kufanya mashambulio ya kulipiza kisasi itakayolenga maslahi yake kutokana na uvamizi wake ndani ya mataifa hizo

Post a Comment

 
Top