Habari
kutoka mji wa Marka zinathibitisha kuwa wanajeshi wa AMISOM wamekutana
na milipuko miwili mikubwa yaliofuatana ndani ya mji wa Marka wakati
walipokuwa wakichota maji mmoja ya visima wa mji huo.
Mashuhuda
wamesema milipuko hizo imewazingira wanajeshi waliokuwa wakitembea kwa
miguu na mmoja ya Magari ya kijeshi,vishindo vya milipuko hizo
zilisikika ndani na nje ya mji wa Marka.
Duru
zinaeleza kuwa Wanajeshi watatu wa Burundi walio sehemu ya wanajeshi
wavamizi wa AMISOM wameuawa kwenye milipuko hizo,habari zaidi zinaeleza
kuwa Baada ya tukio hilo wanajeshi hao Maadui walimpiga risasi mmoja wa
wananchi alipokuwa akitembea katikati ya barabarani wa Marka.
Post a Comment