Trailer ya kwanza ya Furious 7 ilizinduliwa Jumamosi, Nov. 1 na
kuonesha scenes za mwisho za marehemu Paul Walker alizofanya kabla ya
ajali iliyosababisha kifo chake November 2013
Kwenye clip hiyo ya dakika mbili na kitu, Walker aliyekuwa
akijulikana kwenye filamu hiyo kama Brian O’Conner anaonekana akifanya
kile alichokuwa akikipatia – mbio za magari. “Just when you didn’t think
it could get any better,” anasema Walker.
“One last ride,” Vin Diesel anayetumia jina Dominic Toretto anasikika
akimumbia rafiki yake huyo wa kitambo. Walker alifariki akiwa na miaka
40 kwa ajali ya gari huko Santa Clarita, Calif.
Utengenezaji wa filamu hiyo ulisimama kwa muda na baadaye kaka zake
Caleb na Cody waliongezeka kuimalizia. Wengine waliogiza kwenye filamu
hiyo ni Michelle Rodriguez, Jordana Brewster, Dwayne “The Rock” Johnson,
Tyrese Gibson, Ludacris, Elsa Pataky na rapper Iggy Azalea.
Furious 7, itaingia sokoni April 3, 2015.
Home
»
Movie
» Video: Trailer ya kwanza ya Furious 7 yaonesha scenes za mwisho za Paul Walker kabla hajafariki kwa ajali
Subscribe to:
Post Comments (Atom)