0
Muigizaji wa filamu za Bongo , Vincent Kigosi aka Ray amejivunia kuwa sehemu ya waigizaji wa Bongo waliofanikiwa kuliteka soko la filamu la Tanzania na nchi za jirani, ambalo miaka ya nyuma lilimezwa na filamu nyingi za Nigeria.
Ray

“Zamani ukienda katika majumba kuna sinema za kina Ramsey nouah, kina Genevieve nnaji, kina Omotola lakini sasa hivi ukiingia katika majumba ya watu unakuta kina Vincent Kigosi, kina Jay B kina marehemu Steven Kanumba, kwahiyo kiufupi kwamba tasnia tumeweza kubadilisha watanzania wote, sio watanzania tumeweza kutangaza nchi kimataifa,”
alisema Ray katika kipindi cha Kili Chats kinachoongozwa na Gadner G. Habash kupitia EATV.
Ray aliongeza kuwa yeye kwa sasa ni muigizaji mkubwa sio tu kwa Tanzania bali hata nchi za jirani.
“Nikienda Rwanda mimi saivi napokelewa kama rais, nikienda Burundi napokelewa kama rais, Malawi, Congo ndio usiseme kabisa. Kwa hiyo kimsingi tumejaribu kufanya mabadiliko makubwa na kuwashawishi audience wetu kukubali kazi za East Africa kuliko kukubali kazi ambazo ziko mbali huko Nigeria”.

Post a Comment

 
Top