0
Ikiwa ni mwezi mmoja tu tangu aachie wimbo mpya uitwao ‘Upendo’ uliotayarishwa na mshindi wa mtayarishaji bora wa muziki wa kizazi kipya kwenye tuzo za Kilimanjaro mwaka huu, Ben Pol wiki iliyopita aliachia wimbo mpya uitwao ‘Twaendana’ uliotayarishwa na producer wa Arusha, DX.
BenPol_Twaendana
Ben Pol ameiambia Bongo5 kuwa ni kawaida yake kila mwezi wa nane au wa tisa kuachia wimbo wenye mahadhi ya R&B ambayo mashabiki wake wengi wamemzoea akiimba hivyo.
“Hata ukiangalia mwaka jana ilikuwa ‘Wa Ubani’, mwaka juzi ilikuwa ‘Pete’, mwaka wa nyuma yake ilikuwa ‘Numbe 1 Fan’, mwaka wa nyuma yake ulikuwa ‘Nikikupata’,” amesema Ben Pol.
Akizungumzia sababu za kufanya wimbo wa DX, Ben Pol amesema producer huyo wa Arusha ana beats nyingi za R&B kwenye maktaba yake hivyo ilikuwa rahisi wawili hao kupata kitu cha kurekodi.
‘Twaendana’ unapatikana kwenye mtandao wa mkito.com.

Post a Comment

 
Top