Hata hivyo kwa mujibu wa tweets za Mwana FA na Alikiba, huenda zamu ya kuachiwa wimbo huo umekaribia. Kupitia Twitter, shabiki amemuuliza Alikiba lini wataitoa ngoma hiyo aliyoshirikishwa na Mwana FA na kujibu ‘soon’ huku FA naye akiongezea jibu hilo hilo.
Hivi karibuni FA alitweet:
Hii ngoma yangu na Alikiba inaniwasha,NATAKA kuitoa!!lakini…
— Hamis Mwinjuma (@MwanaFA) August 31, 2014
Kwenye mahojiano aliyoyafanya mwezi May mwaka huu na kituo kimoja cha
redio, FA alisema: Watu wengi ambao walikuwa wamezisikia hizi nyimbo
mbili mwanzoni walikuwa wameichagua hiyo na Alikiba ndio iende kwanza na
mi pia nilifikiri hivyo.Lakini ngoma na Alikiba iko na tukienda kufanya video ya hii Mfalme nafikiri tuta shoot na hiyo ya Alikiba pia kwa wakati huo huo tuwe nayo tu kwapani, tukijiskia kwamba watu maskio yao yameshachoka kuskia Mfalme wanataka kitu kingine tutawagonga nayo tu, video inaenda kufanyika Nairobi.”
Post a Comment