Rapper wa kampuni ya Weusi, G-Nako amesema yupo kwenye njia panda kuamua wimbo wake mpya wa kuachia kwakuwa amerekodi nyimbo nyingi na kali.
Kutokana na hali hiyo, rapper huyo wa Arusha aliiambia Bongo5 kuwa anafikiria kutumia watu wengine wamsaidie kuamua wimbo gani anaofaa kuutoa. “Mimi mwenyewe kama nimepagawa fulani, nafikiria kuwa na kamati kunisaidia kuamua ngoma gani natoa maana mimi mwenyewe zinanichanganya,” alisema G-Nako.
Rapper huyo ambaye pamoja na wenzake wa kampuni ya Weusi wakiwemo Joh Makini na Nicki wa Pili wamekuwa wakizunguka kwenye Kili Music Tour 2014, amesema hadi sasa amerekodi nyimbo tano mpya na bado anaendelea kurekodi katika studio mbalimbali.
Amewataja watayarishaji aliofanya nao kazi kwenye nyimbo hizo kuwa ni pamoja na Chizan Brain, Paul Beatz na Nahreel.
Post a Comment