Mjumbe wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Palamagamba
Kabudi (kulia) akizungumza kwenye mdahalo wa Katiba, uliofanyika Dar es
Salaam jana. Picha na Edwin Mjwahuzi
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya
Katiba, Jaji Joseph Warioba na wajumbe wa tume hiyo, jana walitoa
ufafanuzi wa hoja mbalimbali kuhusu mchakato wa Katiba katika mjadala
uliofanyika hapa kiasi cha kuwafanya waliohudhuria siyo tu kumshangilia,
bali walimsindikiza hadi alipoingia kwenye gari lake na wakilifuata na
kulisukuma.
Jaji Warioba na wajumbe wenzake, Profesa
Palamagamba Kabudi, Joseph Butiku, Hamphrey Polepole, Mwantumu Malale na
Awadh Ali Said walitoa ufafanuzi huo katika mdahalo la Katiba
lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere jana.
Jaji Warioba ndiye alianza kuzungumza kwa
kukanusha madai yaliyotolewa juzi katika mdahalo mwingine, kuwa
amepeleka maoni mapya serikalini.
Alisema madai hayo hayana ukweli bali maoni
aliyowasilisha serikalini yalitokana na maoni ya wananchi waliyokusanya
wakati wakiandaa Rasimu ya Kwanza ya Katiba ambayo yataweza kusaidia
katika kuandaa Katiba ya Tanganyika.
Juzi, katika mdahalo uliorushwa na Star TV, Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi
alidai kuwa Jaji Warioba amewasilisha serikalini maoni mapya, ukiacha
yale ambayo yapo katika Rasimu ya Katiba.
Jaji Warioba alisema Tume iliandaa sura ya kwanza
iliyohusu mali na maliasili na sura ya tano kuhusu Serikali ya Muungano
na sura ya nne iliyoelezea serikali za mitaa.
“Sura ya nne na tano tulibaki nazo lakini Machi
27, mwaka huu niliandika barua kwa Waziri wa Katiba na Sheria,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Chikawe (Waziri wa Mambo ya Ndani,
Mathias Chikawe) kwa kuwa alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria kipindi
hicho na nikawakabidhi ili isaidie katika mchakato wa Katiba hasa wakati
wa kuandaa Katiba ya Tanganyika,” alisema Jaji Warioba.
Aliongeza; “Hayakuwa mawazo mapya wala sikupeleka
mawazo mapya, bali ni mawazo tuliyoyakusanya kutoka kwa wananchi na
nimeamua kufanya hivyo kwa kuwa tume kwa kipindi chote ilikuwa wazi na
mimi nimeamua iwe ‘public’ (wazi) kwa kila mmoja kujua, ili iwasaidie
kujua wakati wa uandaaji wa Katiba ya Tanganyika.”
Jaji Warioba pia alifafanua sababu za tume
kupendekeza muundo wa serikali tatu, kwamba haikufanya hivyo kutokana na
idadi ya watu waliotaka muundo huo, bali ilitizama uzito wa hoja
zilizotolewa.
“Wapo wanaosema kuwa idadi ya watu waliotaka
muundo wa serikali tatu ni wachache. Tulipendekeza muundo huo kwa sababu
ya hoja zilizotolewa na siyo wingi au uchache wa waliotoa maoni,”
alisema.
Alisema hoja ya kwanza ni Tanganyika kuvaa koti la
Muungano pia akifafanua jinsi Tanzania Bara inavyoshughulikia masuala
yake ya kiuchumi bila kugusa masuala hayo kwa upande wa Zanzibar.
“Leo hii mawaziri wangapi wa muungano
wanaotembelea Zanzibar kukagua shughuli za maendeleo, pia kuna mgongano
wa Katiba ya Tanzania Bara na Zanzibar. Pia suala la fedha nalo limekuwa
na mvutano kwa muda mrefu hasa kuhusu pande hizi mbili kuwa na akaunti
ya pamoja,” alisema na kuongeza:
“Wajumbe wa tume tulikuwa na itikadi tofauti lakini hata siku
moja hatukuwahi kupiga kura kupitisha jambo lolote, kila
tulichokipendekeza tulikubaliana. Nadhani waendelee na majadiliano ili
wafikie mwafaka,” alisema.
Alisema hata kama mchakato wa Katiba utasitishwa
kwa muda, jambo la msingi linalotakiwa kuheshimiwa ni kuachwa kwa maoni
ya wananchi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba.
Butiku: JK alitetea masilahi ya CCM
Katika mchango wake, Butiku ambaye pia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi wa Mwalimu Nyerere, alisema hotuba ya
Rais Jakaya Kikwete wakati akilifungua Bunge Maalumu la Katiba ililenga
kutetea masilahi ya CCM.
Huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria,
Butiku alisema CCM imeficha maoni ya wananchi yaliyokusanywa na tume
kwa muda wa miezi 18, vikiwamo vitabu mbalimbali vya mapendekezo ya
Watanzania kuhusu nini wanataka kiwemo katika Katiba yao.
Hata hivyo, katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi
aliyoitoa Alhamisi iliyoipita, Rais Kikwete alijivua lawama kuwa ndiye
alikuwa chanzo cha kuvurugika kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Butiku alianza kwa kuuliza, “Nani anaficha maoni”
watu wakaitikia “CCM”, akauliza tena, “Huyu anayeficha maoni
anatuheshimu hatuheshimu,” wasikilizaji wakaitikia, “Hatuheshimu.”
Akijibu kauli ya Rais Kikwete wakati akilifungua
Bunge la Katiba, Butiku alisema: “Unaposema ukweli hutakiwi kuuminya.
Rais Kikwete alisema mashauriano kati yake na wajumbe wa tume hayakuwa
ya kina, lakini ukweli ni kwamba mashauriano yetu yalikuwa ya kina.”
Aliongeza: “Tunaheshimu maoni yake aliyoyatoa ila
kuna maoni aliyotoa yalioonekana kuelekea kuitetea CCM na kama
mnakumbuka katika hotuba yake alikuwa akisisitiza kwamba ‘Tumieni akili
zenu mjadiliane na kupata uamuzi.”
Huku akinukuu baadhi ya vifungu vya Sheria ya
Mabadiliko ya Katiba vinavyoeleza jukumu la Bunge Maalumu la Katiba,
Butiku alisema kilichoandikwa katika Rasimu ya Katiba ni maoni ya
wananchi na ndiyo yanayotakiwa kuheshimiwa kama inavyoeleza sheria hiyo.
“Huu haukuwa mchakato wa kienyeji, nasema wazi
mimi ni mwanachama wa CCM lakini sitarajii Rais awe na kikundi cha
kwenda kuuliza kuhusu utekelezaji wa masuala ya kitaifa. Katika hili CCM
tumekosea,” alisema Butiku.
Aliongeza: “Tume ilitoa vitabu na takwimu
mbalimbali ambazo ziliwekwa katika tovuti ambayo imefungwa. Kuna nyaraka
mbalimbali ambazo Tume ilizikusanya baada ya kukusanya maoni lakini
zimefichwa.”
Akizungumza kwa njia ya kuuliza zaidi maswali, Butiku alisema
kama muundo wa serikali tatu umekuwa na mgogoro je, ni sawa kuwa na
muundo wa serikali mbili wenye nchi mbili?
Alisema hakuna aliyekataa muundo wa serikali
mbili, ila muundo huo unatakiwa kufanyiwa maboresho makubwa ambayo
utekelezaji wake ndiyo tatizo... “Inakuwaje leo watu wazima tunabishana
jambo lililo wazi kabisa wakati suluhisho tunalijua?”
Polepole na gharama za serikali tatu
Polepole ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi za
Kiraia alisema kauli ambazo zinatolewa kuhusu gharama za kuendesha
serikali tatu hazina ukweli wowote kwani katika rasimu hiyo wamebainisha
vyanzo vya mapato.
Polepole alisema waliiandikia barua Hazina kuomba
taarifa zitakazotumika kuendesha Serikali ya Muungano na kwa mwaka
2011/12 bajeti ilikuwa Sh1.4 trilioni, mwaka 2012/13 (Sh1.8 trilioni) na
mwaka 2013/14 ni Sh1.9 trilioni.
“Kwa kiwango hiki, Serikali ya Muungano haitakuwa
na gharama zozote zile za ziada na kinachojitokeza sasa ni tatizo la
masilahi binafsi,” alisema Polepole na kuongeza: “Watu wanataka serikali
mbili kwa sababu ina mambo yote ya Muungano na Tanganyika kwa sababu
ndiyo inayoteua wakurugenzi, makatibu wakuu na wengineo, hivyo wakipata
urais wanalipana fadhila.”
Alisema wakati wakikusanya maoni, makatibu wakuu
wa Serikali ya Zanzibar walipendekeza serikali tatu, kamati ya makatibu
wakuu Serikali ya Muungano walipendekeza serikali mbili lakini
zilizoongezwa mambo ya Muungano.
Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia
mambo yote ya Tanzania bara ilipendekeza serikali tatu na Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano iliyopewa dhamana ya kuimarisha Muungano
ilipendekeza serikali tatu.
“Kwa hali yoyote ile huwezi kuepuka mapendekezo
yaliyomo katika Rasimu kwani yataondoa kero zilizopo kwa pande zote,”
alisema Polepole.
Kabudi atoa somo
Akitoa mchango wake, Profesa Kabudi alisema: “Nchi
hii ni kubwa kuliko sisi sote, hakuna mkubwa zaidi ya nchi hii, sisi
sote tutakufa, tutazikwa na tutaoza lakini nchi hii itaendelea kuwapo.”
Alisema kuhusu Muungano, Wazanzibari wanazungumza
kuliko Watanganyika, lakini ukifika wakati Watanganyika wakazungumza,
itakuwa hatari hivyo akasema ufike wakati Watanganyika wapewe serikali
yao wakati wakiogopa, wasisubiri waanze kuidai Tanganyika yao.
Alisema baada ya kuvurugwa kwa Kongo, Tanzania ndiyo imekuwa
kama nyonga ya Afrika na kuwa na umuhimu wa kipekee kwa ulinzi wa nchi
nane zilizoizunguka na Bahari ya Hindi.
Alishangazwa na hatua ya kuwekwa kando kwa tume
baada tu ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba na kwamba hatua hiyo ndiyo
chanzo cha mkwamo uliopo kwa sasa kwa kuwa ndiyo iliyokuwa ikijua chanzo
na kila ibara na sababu za kuwapo kwake, hivyo ingeweza kutoa ufafanuzi
pale ambako litatokea tatizo.
Wakati akitoa kauli hiyo, watu waliofurika katika
ukumbi huo walilipuka kwa shangwe, “Sema usiogope sema,” huku Profesa
huyo akihitimisha kwa kuwataka Watanzania kujadili mambo hayo kwa ajili
ya mustakabali wa Taifa.
Awadh azungumzia misukosuko
Awadh ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) alisema Muungano umefika hapa baada ya kupitia misukosuko mingi.
“Hakuna sehemu Tume iliambiwa itumie takwimu, bali
ni hoja zinazofanana na kutofautiana na kufanya uamuzi, ndicho ambacho
tulikuwa tukikifanya wakati wote,” alisema na kuongeza: “Watu wengi
suala la muungano hawalielewi na wanaupotosha umma. Muungano unatakiwa
kuweka haki sawa, fursa sawa na hadhi sawa, lakini usipokuwa na haya
hatuwezi kuwa na muungano imara.”
Alitoa angalizo kwa wanasiasa kuzungumza kama
wachumi hasa katika gharama, jambo ambalo hawana uzoefu na uelewa nalo
akisema wanaongeza vitu visivyo na ukweli ndani yake.
Malale: Hatuwezi kutumia maoni kama kichaka
Malale alisema kuwa Tume ilikusanya maoni ya
wananchi nchi nzima na kamwe haiwezi kuyatumia kama kichaka, kama
wanavyofanya watu wengine.
“Watu waache kutumia maoni ya wananchi kama
kichaka cha hoja zao. Tume imechukua maoni ya wananchi na kuyaweka kwa
pamoja. Maoni yao yanatakiwa kuheshimiwa na yasitumike kama kichaka kwa
wengine,” alisema Malale.
Jaji Warioba alihitimisha mdahalo huo kwa kuwajibu
wanasiasa wanaodai kuwa takwimu za idadi ya wananchi waliotoa maoni si
sahihi kutokana na idadi kupishana kati ya Mkoa wa Kigoma na Tabora.
“Kwani wananchi wa Kigoma siyo Watanzania? Jumla
ya wananchi 8,600 walitoa maoni mkoani Kigoma na wananchi 3,011 mkoani
Tabora,” alisema na kuongeza: “Mkoa wa Kigoma na Kagera ndiyo iliyoko
pembezoni, hivyo ina matatizo lukuki ndiyo maana walijitokeza kutoa
maoni kwa wingi ili yaingizwe katika Katiba.”
Alisisitiza kuwa hata kama yatazungumzwa maneno gani, Tume ya
Mabadiliko ya Katiba ndiyo iliyohoji wananchi, hivyo inajua kila jambo
walilopendekeza na kipi ambacho wananchi wanakitaka.
Alipoulizwa nini hatma ya Bunge Maalumu la Katiba
kutokana na baadhi ya wajumbe wake kususia vikao vyake alisema:
“Nawashauri waache masilahi binafsi ya makundi yao na wafanye kazi.
Wajifiche chumbani na wapate mwafaka wa kuijadili rasimu.
Fidelis Butahe na Ibrahim Yamola, Mwananchi
Dar es Salaam. Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya
Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba na wajumbe wa tume hiyo, jana
walitoa ufafanuzi wa hoja mbalimbali kuhusu mchakato wa Katiba katika
mjadala uliofanyika hapa kiasi cha kuwafanya waliohudhuria siyo tu
kumshangilia, bali walimsindikiza hadi alipoingia kwenye gari lake na
wakilifuata na kulisukuma.
Jaji Warioba na wajumbe wenzake, Profesa
Palamagamba Kabudi, Joseph Butiku, Hamphrey Polepole, Mwantumu Malale na
Awadh Ali Said walitoa ufafanuzi huo katika mdahalo la Katiba
lililoandaliwa na Taasisi ya Mwalimu Nyerere jana.
Jaji Warioba ndiye alianza kuzungumza kwa
kukanusha madai yaliyotolewa juzi katika mdahalo mwingine, kuwa
amepeleka maoni mapya serikalini.
Alisema madai hayo hayana ukweli bali maoni
aliyowasilisha serikalini yalitokana na maoni ya wananchi waliyokusanya
wakati wakiandaa Rasimu ya Kwanza ya Katiba ambayo yataweza kusaidia
katika kuandaa Katiba ya Tanganyika.
Juzi, katika mdahalo uliorushwa na Star TV, Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi
alidai kuwa Jaji Warioba amewasilisha serikalini maoni mapya, ukiacha
yale ambayo yapo katika Rasimu ya Katiba.
Jaji Warioba alisema Tume iliandaa sura ya kwanza
iliyohusu mali na maliasili na sura ya tano kuhusu Serikali ya Muungano
na sura ya nne iliyoelezea serikali za mitaa.
“Sura ya nne na tano tulibaki nazo lakini Machi
27, mwaka huu niliandika barua kwa Waziri wa Katiba na Sheria,
Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Chikawe (Waziri wa Mambo ya Ndani,
Mathias Chikawe) kwa kuwa alikuwa Waziri wa Katiba na Sheria kipindi
hicho na nikawakabidhi ili isaidie katika mchakato wa Katiba hasa wakati
wa kuandaa Katiba ya Tanganyika,” alisema Jaji Warioba.
Aliongeza; “Hayakuwa mawazo mapya wala sikupeleka
mawazo mapya, bali ni mawazo tuliyoyakusanya kutoka kwa wananchi na
nimeamua kufanya hivyo kwa kuwa tume kwa kipindi chote ilikuwa wazi na
mimi nimeamua iwe ‘public’ (wazi) kwa kila mmoja kujua, ili iwasaidie
kujua wakati wa uandaaji wa Katiba ya Tanganyika.”
Jaji Warioba pia alifafanua sababu za tume
kupendekeza muundo wa serikali tatu, kwamba haikufanya hivyo kutokana na
idadi ya watu waliotaka muundo huo, bali ilitizama uzito wa hoja
zilizotolewa.
“Wapo wanaosema kuwa idadi ya watu waliotaka muundo wa serikali
tatu ni wachache. Tulipendekeza muundo huo kwa sababu ya hoja
zilizotolewa na siyo wingi au uchache wa waliotoa maoni,” alisema.
Alisema hoja ya kwanza ni Tanganyika kuvaa koti la
Muungano pia akifafanua jinsi Tanzania Bara inavyoshughulikia masuala
yake ya kiuchumi bila kugusa masuala hayo kwa upande wa Zanzibar.
“Leo hii mawaziri wangapi wa muungano
wanaotembelea Zanzibar kukagua shughuli za maendeleo, pia kuna mgongano
wa Katiba ya Tanzania Bara na Zanzibar. Pia suala la fedha nalo limekuwa
na mvutano kwa muda mrefu hasa kuhusu pande hizi mbili kuwa na akaunti
ya pamoja,” alisema na kuongeza:
“Wajumbe wa tume tulikuwa na itikadi tofauti
lakini hata siku moja hatukuwahi kupiga kura kupitisha jambo lolote,
kila tulichokipendekeza tulikubaliana. Nadhani waendelee na majadiliano
ili wafikie mwafaka,” alisema.
Alisema hata kama mchakato wa Katiba utasitishwa
kwa muda, jambo la msingi linalotakiwa kuheshimiwa ni kuachwa kwa maoni
ya wananchi yaliyomo katika Rasimu ya Katiba.
Butiku: JK alitetea masilahi ya CCM
Katika mchango wake, Butiku ambaye pia ni
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi wa Mwalimu Nyerere, alisema hotuba ya
Rais Jakaya Kikwete wakati akilifungua Bunge Maalumu la Katiba ililenga
kutetea masilahi ya CCM.
Huku akishangiliwa na mamia ya watu waliohudhuria,
Butiku alisema CCM imeficha maoni ya wananchi yaliyokusanywa na tume
kwa muda wa miezi 18, vikiwamo vitabu mbalimbali vya mapendekezo ya
Watanzania kuhusu nini wanataka kiwemo katika Katiba yao.
Hata hivyo, katika hotuba yake ya mwisho wa mwezi
aliyoitoa Alhamisi iliyoipita, Rais Kikwete alijivua lawama kuwa ndiye
alikuwa chanzo cha kuvurugika kwa mchakato wa kupata Katiba Mpya.
Butiku alianza kwa kuuliza, “Nani anaficha maoni”
watu wakaitikia “CCM”, akauliza tena, “Huyu anayeficha maoni
anatuheshimu hatuheshimu,” wasikilizaji wakaitikia, “Hatuheshimu.”
Akijibu kauli ya Rais Kikwete wakati akilifungua
Bunge la Katiba, Butiku alisema: “Unaposema ukweli hutakiwi kuuminya.
Rais Kikwete alisema mashauriano kati yake na wajumbe wa tume hayakuwa
ya kina, lakini ukweli ni kwamba mashauriano yetu yalikuwa ya kina.”
Aliongeza: “Tunaheshimu maoni yake aliyoyatoa ila
kuna maoni aliyotoa yalioonekana kuelekea kuitetea CCM na kama
mnakumbuka katika hotuba yake alikuwa akisisitiza kwamba ‘Tumieni akili
zenu mjadiliane na kupata uamuzi.”
Huku akinukuu baadhi ya vifungu vya Sheria ya Mabadiliko ya
Katiba vinavyoeleza jukumu la Bunge Maalumu la Katiba, Butiku alisema
kilichoandikwa katika Rasimu ya Katiba ni maoni ya wananchi na ndiyo
yanayotakiwa kuheshimiwa kama inavyoeleza sheria hiyo.
“Huu haukuwa mchakato wa kienyeji, nasema wazi
mimi ni mwanachama wa CCM lakini sitarajii Rais awe na kikundi cha
kwenda kuuliza kuhusu utekelezaji wa masuala ya kitaifa. Katika hili CCM
tumekosea,” alisema Butiku.
Aliongeza: “Tume ilitoa vitabu na takwimu
mbalimbali ambazo ziliwekwa katika tovuti ambayo imefungwa. Kuna nyaraka
mbalimbali ambazo Tume ilizikusanya baada ya kukusanya maoni lakini
zimefichwa.”
Akizungumza kwa njia ya kuuliza zaidi maswali,
Butiku alisema kama muundo wa serikali tatu umekuwa na mgogoro je, ni
sawa kuwa na muundo wa serikali mbili wenye nchi mbili?
Alisema hakuna aliyekataa muundo wa serikali
mbili, ila muundo huo unatakiwa kufanyiwa maboresho makubwa ambayo
utekelezaji wake ndiyo tatizo... “Inakuwaje leo watu wazima tunabishana
jambo lililo wazi kabisa wakati suluhisho tunalijua?”
Polepole na gharama za serikali tatu
Polepole ambaye pia ni Mwenyekiti wa Asasi za
Kiraia alisema kauli ambazo zinatolewa kuhusu gharama za kuendesha
serikali tatu hazina ukweli wowote kwani katika rasimu hiyo wamebainisha
vyanzo vya mapato.
Polepole alisema waliiandikia barua Hazina kuomba
taarifa zitakazotumika kuendesha Serikali ya Muungano na kwa mwaka
2011/12 bajeti ilikuwa Sh1.4 trilioni, mwaka 2012/13 (Sh1.8 trilioni) na
mwaka 2013/14 ni Sh1.9 trilioni.
“Kwa kiwango hiki, Serikali ya Muungano haitakuwa
na gharama zozote zile za ziada na kinachojitokeza sasa ni tatizo la
masilahi binafsi,” alisema Polepole na kuongeza: “Watu wanataka serikali
mbili kwa sababu ina mambo yote ya Muungano na Tanganyika kwa sababu
ndiyo inayoteua wakurugenzi, makatibu wakuu na wengineo, hivyo wakipata
urais wanalipana fadhila.”
Alisema wakati wakikusanya maoni, makatibu wakuu
wa Serikali ya Zanzibar walipendekeza serikali tatu, kamati ya makatibu
wakuu Serikali ya Muungano walipendekeza serikali mbili lakini
zilizoongezwa mambo ya Muungano.
Alisema Ofisi ya Waziri Mkuu inayoshughulikia
mambo yote ya Tanzania bara ilipendekeza serikali tatu na Ofisi ya
Makamu wa Rais Muungano iliyopewa dhamana ya kuimarisha Muungano
ilipendekeza serikali tatu.
“Kwa hali yoyote ile huwezi kuepuka mapendekezo
yaliyomo katika Rasimu kwani yataondoa kero zilizopo kwa pande zote,”
alisema Polepole.
Kabudi atoa somo
Akitoa mchango wake, Profesa Kabudi alisema: “Nchi
hii ni kubwa kuliko sisi sote, hakuna mkubwa zaidi ya nchi hii, sisi
sote tutakufa, tutazikwa na tutaoza lakini nchi hii itaendelea kuwapo.”
Alisema kuhusu Muungano, Wazanzibari wanazungumza
kuliko Watanganyika, lakini ukifika wakati Watanganyika wakazungumza,
itakuwa hatari hivyo akasema ufike wakati Watanganyika wapewe serikali
yao wakati wakiogopa, wasisubiri waanze kuidai Tanganyika yao.
Alisema baada ya kuvurugwa kwa Kongo, Tanzania
ndiyo imekuwa kama nyonga ya Afrika na kuwa na umuhimu wa kipekee kwa
ulinzi wa nchi nane zilizoizunguka na Bahari ya Hindi.
Alishangazwa na hatua ya kuwekwa kando kwa tume
baada tu ya kuwasilisha Rasimu ya Katiba na kwamba hatua hiyo ndiyo
chanzo cha mkwamo uliopo kwa sasa kwa kuwa ndiyo iliyokuwa ikijua chanzo
na kila ibara na sababu za kuwapo kwake, hivyo ingeweza kutoa ufafanuzi
pale ambako litatokea tatizo.
Wakati akitoa kauli hiyo, watu waliofurika katika
ukumbi huo walilipuka kwa shangwe, “Sema usiogope sema,” huku Profesa
huyo akihitimisha kwa kuwataka Watanzania kujadili mambo hayo kwa ajili
ya mustakabali wa Taifa.
Awadh azungumzia misukosuko
Awadh ambaye ni Rais wa Chama cha Wanasheria Zanzibar (ZLS) alisema Muungano umefika hapa baada ya kupitia misukosuko mingi.
“Hakuna sehemu Tume iliambiwa itumie takwimu, bali
ni hoja zinazofanana na kutofautiana na kufanya uamuzi, ndicho ambacho
tulikuwa tukikifanya wakati wote,” alisema na kuongeza: “Watu wengi
suala la muungano hawalielewi na wanaupotosha umma. Muungano unatakiwa
kuweka haki sawa, fursa sawa na hadhi sawa, lakini usipokuwa na haya
hatuwezi kuwa na muungano imara.”
Alitoa angalizo kwa wanasiasa kuzungumza kama
wachumi hasa katika gharama, jambo ambalo hawana uzoefu na uelewa nalo
akisema wanaongeza vitu visivyo na ukweli ndani yake.
Malale: Hatuwezi kutumia maoni kama kichaka
Malale alisema kuwa Tume ilikusanya maoni ya
wananchi nchi nzima na kamwe haiwezi kuyatumia kama kichaka, kama
wanavyofanya watu wengine.
“Watu waache kutumia maoni ya wananchi kama kichaka cha hoja
zao. Tume imechukua maoni ya wananchi na kuyaweka kwa pamoja. Maoni yao
yanatakiwa kuheshimiwa na yasitumike kama kichaka kwa wengine,” alisema
Malale.
Jaji Warioba alihitimisha mdahalo huo kwa kuwajibu
wanasiasa wanaodai kuwa takwimu za idadi ya wananchi waliotoa maoni si
sahihi kutokana na idadi kupishana kati ya Mkoa wa Kigoma na Tabora.
“Kwani wananchi wa Kigoma siyo Watanzania? Jumla
ya wananchi 8,600 walitoa maoni mkoani Kigoma na wananchi 3,011 mkoani
Tabora,” alisema na kuongeza: “Mkoa wa Kigoma na Kagera ndiyo iliyoko
pembezoni, hivyo ina matatizo lukuki ndiyo maana walijitokeza kutoa
maoni kwa wingi ili yaingizwe katika Katiba.”
Alisisitiza kuwa hata kama yatazungumzwa maneno
gani, Tume ya Mabadiliko ya Katiba ndiyo iliyohoji wananchi, hivyo
inajua kila jambo walilopendekeza na kipi ambacho wananchi wanakitaka.

Post a Comment