0

Wateja wakinunua nyama ya ng’ombe  ndani ya machinjio ya Vingunguti, Dar es Salaam. Rafael Lubava  

Dar es Salaam. Ukiwa unakaribia  katika eneo la machinjio lililopo Vingunguti jijini hapa kabla ya kuingia ndani salamu ya kwanza utakayopokelewa nayo ni “Karibu mteja   fungu  moja ni Sh 1,000 tu…dada karibu uboreshe ndoa…kaka karibu uboreshe ndoa,”hizo ni sauti za vijana waliopanga bidhaa zao kwenye meza pembezoni mwa Barabara ya Vingunguti, nje ya banda la kuchinjia mifugo.
Lakini licha ya salamu yao nzuri ya ukarimu iliyojaa mbwembwe nyingi, huenda ukashindwa kuitikia kutokana na harufu mbaya na hewa nzito iliyozingira anga la hapa. Unaweza ukawa unazuia ile hewa isiingie ndani ya kinywa chako. Ukaziba mdomo na pua kidogo kuruhusu hewa kiasi kupita. Ila kwa wenyeji wa hapa inaonekana hilo siyo tatizo kwao, wanaendelea kupiga mzigo. Wengine wanapata vifungua kinywa bila wasiwasi.
Salamu hiyo ndiyo kivuto kwa wateja. Hii ndiyo chachu kwao ili wasogee karibu kupata huduma hiyo, hasa wakinamama. Na ndivyo na mimi nilivyovutiwa na kusogea karibu kutaka kufahamu undani wa bidhaa hizo.
Ilipofika saa moja kasoro asubuhi. Hapa kila mmoja anajitahidi kuhakikisha anamvutia mteja kwa upande wake.
Lengo ikiwa ni mteja hapiti bila kununua  chochote. Japo kuna wakati mwingine hali huwa tofauti kwani  si kila anayepita barabarani  hapo huwa na lengo la kununua nyama, wengine ni wapita njia tu. Ndiyo biashara.
Kama mmoja wa wapitanjia ambaye niligeuka kuwa mteja nilisogea karibu. Nilitaka kufahamu undani wa bidhaa hizi. Shauku hiyo haikuja hivihivi bali ni kutokana na maneno  ambayo yanasemwa mitaani.
Ukipita mitaani utasikia watu wakisema mambo mengi juu ya machinjioni. Baadhi husema kuwa kuna watu kazi yao ni kuokota baadhi ya masalia ya nyama za ng’ombe. Wakishaokota mabaki hayo huyauza kwa bei  ndogo ukilinganisha na ile ya buchani.
Kwa sasa kilo moja   nyama huuzwa kwa Sh5,000 hadi Sh 6,000. Bei ya hawa jamaa ni tofauti kidogo. Unafuu wa bei yao hautokani na yale madai kuwa wao huokota masalia na kwenda kuuzia watu iwe nje ya machinjio ua sehemu nyingine huko mitaani. Wanasema sababu ni kuwa wao wapo kiwandani.
Maneno hayo ananiambia kijana mmoja anayeuza nyama nje ya machinjio hayo aliyejitambulisha kwa jina la Daniel Lucas. Ni mmoja kati ya vijana wachacharikaji kweli ambao wamepanga mstari wa meza zenye mafungu ya nyama tofauti.
Juu ya meza kila moja kuna mafungu kama kumi hivi ya nyama. Wengine wameweka  nyama za utumbo, wengine steki na wengine maini. Wakati huo pilika za kuwahudumia wateja zinaendelea. Vijana wengine wanaonekana kuwahudumia huku wengine wakiendelea kukata nyama na kuzipanga mezani.
Chini ya kila meza kuna ndoo yenye maji ndani yake kuna  nyama. Ikabidi nihoji kwanini wanafanya hivyo, “Huwa tunasafisha nyama kabla ya kuzipanga mezani. Wakati mwingine tunanyunyizia hayo maji kwenye nyama ili zisiharibike kama siku hiyo hakuna wateja na nyama ikachelewa kuisha,” anasema Lucas. Baada ya kusonga karibu ili kujionea nyama hizo na maji. Mazingira ya pale hayakuwa rafiki sana  kwa maana ya usalama wa afya ya mlaji.
Majibu hayo bado si ya kuridhika nayo kutokana na ile hali ya usafi wa eneo lile. Ile hali ya kumwaga maji inafanya chini kuwe na matope, inzi  lakini wao hawaonekani kujalii ile hali hata kidogo. Pia mimi pia napiga moyo konde naendelea kuka nao kwa muda wa dakika kadhaa.
Wateja wanakuja na kuondoka. Kuna wanaokuja na kuuliza. Wengine wanauliza bei na kununua. Kwa wanunuaji, akichukua fungu moja au mawili ya nyama anawekewa kwenye mfuko mweusi na kuondoka.
Lucas anasema kwa malipo ya kila fungu la nyama ya  utumbo ni Sh1,000. Hapa hakuna kupunguziwa. Hakuna kipimo. Kipimo wanakijua wao wenyewe. Ila kwa wanunuaji kipimo ni macho yao. Licha ya kuwa macho yanaweza kudanganya. Mizani ndiyo ingekuwa wakili pekee na msema kweli na mtenda haki hapa, lakini kwa wafanyabiashara wa hapa hali siyo hivyo.
Kwa upande wa nyama ya steki kijana huyo anasema kuwa fungu moja ni Sh2,000. Mfumo ule ule, hakuna mizani. Mafungu yamewekwa kazi ni kwako mteja kuchagua fungu ambalo unapendezwa nalo.
Namuuliza huyu kijana  kwa nini hawapimi nyama kwa kutumia mizani.
“Unajua dada haya mafungu tunayoweka hapa  bei yake ni sawa na bure…Sisi ni kama tunagawa tu nyama kwa wateja wetu. Wee nenda ukapime hilo fungu moja ulilochukua halafu ukirudi utatuambia. Kama ingekuwa tunapunja tusingekuwa tunapata wateja…kwanza mashine ni mizingo tu hapa  tutaweka wapi mazingira yenyewe si unayaona,”alijitetea Lucas kwa ujasiri.
Niliposogea mezani vilivyokuwa vimemwagwa vipande vya steki hali ilikuwa ilele. Kilichonifurahisha kwa upande wa steki. Ukifika hawa vijana wanahakikisha wamekupa mfuko wa plastiki. Huo mfuko unavaa mkononi kabla ya kuanza kuchagua kipande cha nyama. Tofauti na kwenye utumbo. Hapa usafi kidogo unazingatiwa.
Kwenye maini nako ni kama kule kwa utumbo. Unachagua kipande na kulipia Sh2,000 kisha unaondoka.
Wanunuaji wengine ndiyo wale wanaoonekana pembeni wakiwa katika pilikapilika za  kutengeneza mishikaki na kuchemsha supu. Mishikaki   na supu huenda sambamba na mihogo ambayo inakaangwa na kinamama wa hapa. Kama ni mgeni wa hili eneo kwa mara ya kwanza lazima utajiuliza maswali mengi kabla ya kuchukua uamuzi wa kukaa na kutia kitu chochote kinywani.
Mazingira ambayo vitu hivi vinatengenezwa siyo mazuri kwa afya hata kidogo. Kwanza ile hali ya unyevunyevu, matope na inzi wanaozunguka kila kona ya eneo hilo la machinjio. Asili tu ya eneo hilo inatosha kulifanya kuwe na harufu ambayo inachangia kuwapo kwa inzi wengi. Baadhi ya sehemu zina vinyesi vya wanyama ambao wameletwa kwa ajili ya kuchinjwa.
Bado eneo hilo hilo watu wanatumia kufanya  biashara ya chakula. Pia watu wameketi wanakula na kunywa.
Wafanyabishara hao wengine wamegawanyika katika makundi matatu. Wakaanga mihogo, wauza supu pamoja na chapati na maandazi, pombe za kisasa na kienyeji, wauza nyanya vitunguu na mbogamboga nyingine na waendesha bodaboda. Hawa wapo sambamba na wateja wao pia.
Wateja wamekaa katika makundi. Kwenye mabenchi. Kuna wanaokula mihogo, kuna wa chapati na supu. Pombe za kienyeji ile ya kule uchagani mbege.Walionifurahisha ni wale waliokuwa wanakunywa bia. Walikuwa wamekaa kwenye benchi pia. Kila kundi la watu watatu au wanne walikuwa na kreti lao la bia, wamekaa kwenye kona.
Dar es Salaam. Ukiwa unakaribia  katika eneo la machinjio lililopo Vingunguti jijini hapa kabla ya kuingia ndani salamu ya kwanza utakayopokelewa nayo ni “Karibu mteja   fungu  moja ni Sh 1,000 tu…dada karibu uboreshe ndoa…kaka karibu uboreshe ndoa,”hizo ni sauti za vijana waliopanga bidhaa zao kwenye meza pembezoni mwa Barabara ya Vingunguti, nje ya banda la kuchinjia mifugo.
Lakini licha ya salamu yao nzuri ya ukarimu iliyojaa mbwembwe nyingi, huenda ukashindwa kuitikia kutokana na harufu mbaya na hewa nzito iliyozingira anga la hapa. Unaweza ukawa unazuia ile hewa isiingie ndani ya kinywa chako. Ukaziba mdomo na pua kidogo kuruhusu hewa kiasi kupita. Ila kwa wenyeji wa hapa inaonekana hilo siyo tatizo kwao, wanaendelea kupiga mzigo. Wengine wanapata vifungua kinywa bila wasiwasi.
Salamu hiyo ndiyo kivuto kwa wateja. Hii ndiyo chachu kwao ili wasogee karibu kupata huduma hiyo, hasa wakinamama. Na ndivyo na mimi nilivyovutiwa na kusogea karibu kutaka kufahamu undani wa bidhaa hizo.
Ilipofika saa moja kasoro asubuhi. Hapa kila mmoja anajitahidi kuhakikisha anamvutia mteja kwa upande wake.
Lengo ikiwa ni mteja hapiti bila kununua  chochote. Japo kuna wakati mwingine hali huwa tofauti kwani  si kila anayepita barabarani  hapo huwa na lengo la kununua nyama, wengine ni wapita njia tu. Ndiyo biashara.
Kama mmoja wa wapitanjia ambaye niligeuka kuwa mteja nilisogea karibu. Nilitaka kufahamu undani wa bidhaa hizi. Shauku hiyo haikuja hivihivi bali ni kutokana na maneno  ambayo yanasemwa mitaani.
Ukipita mitaani utasikia watu wakisema mambo mengi juu ya machinjioni. Baadhi husema kuwa kuna watu kazi yao ni kuokota baadhi ya masalia ya nyama za ng’ombe. Wakishaokota mabaki hayo huyauza kwa bei  ndogo ukilinganisha na ile ya buchani.
Kwa sasa kilo moja   nyama huuzwa kwa Sh5,000 hadi Sh 6,000. Bei ya hawa jamaa ni tofauti kidogo. Unafuu wa bei yao hautokani na yale madai kuwa wao huokota masalia na kwenda kuuzia watu iwe nje ya machinjio ua sehemu nyingine huko mitaani. Wanasema sababu ni kuwa wao wapo kiwandani.
Maneno hayo ananiambia kijana mmoja anayeuza nyama nje ya machinjio hayo aliyejitambulisha kwa jina la Daniel Lucas. Ni mmoja kati ya vijana wachacharikaji kweli ambao wamepanga mstari wa meza zenye mafungu ya nyama tofauti.
Juu ya meza kila moja kuna mafungu kama kumi hivi ya nyama. Wengine wameweka  nyama za utumbo, wengine steki na wengine maini. Wakati huo pilika za kuwahudumia wateja zinaendelea. Vijana wengine wanaonekana kuwahudumia huku wengine wakiendelea kukata nyama na kuzipanga mezani.
Chini ya kila meza kuna ndoo yenye maji ndani yake kuna  nyama. Ikabidi nihoji kwanini wanafanya hivyo, “Huwa tunasafisha nyama kabla ya kuzipanga mezani. Wakati mwingine tunanyunyizia hayo maji kwenye nyama ili zisiharibike kama siku hiyo hakuna wateja na nyama ikachelewa kuisha,” anasema Lucas. Baada ya kusonga karibu ili kujionea nyama hizo na maji. Mazingira ya pale hayakuwa rafiki sana  kwa maana ya usalama wa afya ya mlaji.
Majibu hayo bado si ya kuridhika nayo kutokana na ile hali ya usafi wa eneo lile. Ile hali ya kumwaga maji inafanya chini kuwe na matope, inzi  lakini wao hawaonekani kujalii ile hali hata kidogo. Pia mimi pia napiga moyo konde naendelea kuka nao kwa muda wa dakika kadhaa.

Post a Comment

Top