Dar es Salaam. Timu ya taifa ya soka ya vijana chini ya miaka
17, Ngorongoro Heroes imeshindwa kutamba mbele ya wenzao wa Afrika
Kusini, baada ya kulazimishwa suluhu nyumbani.
Katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam
Complex, Chamazi, Dar es Salaam, ulikuwa na nafasi kadhaa za kufunga kwa
kila timu lakini zilitumiwa vibaya.
Mchezo huo ni wa kuwania nafasi ya kufuzu kwa
fainali za Afrika kwa vijana wa umri huo zitakazofanyika Niger, ambapo
mchezo wa marudiano utapigwa nchini Afrika Kusini baada ya wiki mbili.
Serengeti Boys walianza vizuri katika kipindi cha
kwanza, lakini nafasi zilikuwa chache na nzuri kupitia kwa Athanas
Mdamu, ambaye alionekana huenda angeweza kuitoa Tanzania kimasomaso.
Licha ya kupata nafasi kadhaa katika kipindi cha
kwanza, hali hiyo haikusaidia hata katika kipindi cha pili, wakati
Khanyiso Mayo wa Afrika Kusini akionekana kuwa msumbufu, lakini uimara
wa kipa wa Serengeti, Metacha Mnata alifanya kazi ya ziada.
Post a Comment