Mkinga. Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Chiku Gallawa
ameishangaa Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga kuweka ushuru wa mkaa kama
eneo la ukusanyaji wa mapato ya ndani na kutaka biashara hiyo ikome kwa
sababu madhara yake ni makubwa katika uharibifu wa mazingira.
Alisema hayo alipokutana na wakuu wa idara pamoja na madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo.
Gallawa aliwataka wakuu wa idara pamoja na
wataalamu wa halmashauri hiyo kutumia elimu zao kubuni njia za
kuwaongezea vipato wananchi ili hatimaye wawe na uwezo wakuchangia
shughuli za maendeleo. “Haiwezekani, halmashauri iweke katika mipango
yake ushuru wa mkaa na kuni kama sehemu ya mapato, yaani inabariki
uharibifu wa mazingira kwa makusanyo ya siku chache yatakayosababisha
jangwa la kudumu,” alihoji Gallawa.
Post a Comment