Bado kuna ubishi mwingi kwa mashabiki wa soka kuhusu ubora wa mabeki wa pembeni wanaocheza Ligi Kuu Bara.
Wengi wanaamini beki wa kulia wa zamani wa Yanga,
Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’ ndiye aliwahi kuitendea haki nafasi ya beki wa
pembeni. Mchezaji mwingine anayetajwa kuitendea haki nafasi ya ulinzi ni
beki wa zamani wa Simba, Shomari Kapombe.
Kapombe ambaye sasa ataichezea Azam kwenye Ligi
Kuu Bara msimu ujao aliwahi kufanya majaribio kwenye klabu ya AS Cannes
Ufaransa.
Akizungumzia majaribio hayo, Kapombe
anasema,“Nilichukuliwa hapa kwenda Uholanzi kufanya majaribio, lakini
nilipofika nikapata nafasi Ufaransa kwenye timu ya AS Cannes nikafanya
majaribio siku tatu na ile timu ikakubalina na mimi kwamba wanisajili.
“Lakini kilichokuja kutokea baadaye ni kwamba
walivunja makubaliano yetu kwani wao walikubaliana na Simba wanitoe mimi
bure halafu nikiuzwa kwenye timu nyingine ndipo Simba watapata asilimia
fulani na kweli nikasaini miaka miwili, lakini ile timu haikufanya kama
vile tulivyokubalina kwenye mkataba hasa katika mshahara,”anasema
Kapombe.
Anasema,”Ujue lilipotokea lile tatizo ilinichukua
muda mrefu kuamua na wakati huo huo nilikuwa namsikiliza kwanza wakala
wangu, pia Simba walikuwa wanakuja kunishauri, lakini wengi walinishauri
nirudi katika ile timu mimi nikawaambia nitawezaje kurudi sehemu ambayo
sipati maslahi yangu yaliyokuwa kwenye mkataba? na uzuri mkataba
unaongea kila kitu hivyo hayo ni matatizo ya hiyo timu sio mimi,”
anasema Kapombe.
“Matatizo yaliyotokea kule ni mambo ya mshahara,
lakini mimi Kapombe nacheza mpira kama kama kazi kwani kuna watu nyuma
yangu wananiangalia, familia yangu yote inaniangalia mimi ndio maana
nilienda AS Cannes kwa lengo la kuisaidia familia yangu, nisingeweza
kuvumilia kuishi bila mshahara nikaamua kurudi nyumbani na kujiunga na
Azam,”anasema Kapombe.
Post a Comment