JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO
PRESS RELEASE
Siku ya Kimataifa ya Familia huadhimishwa
kila mwaka tarehe 15 Mei na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.
Maadhimisho hayo yanatokana na tamko la Baraza la Umoja wa Mataifa Na.
47/237 la tarehe 20 Septemba, 1993, linalotaka Jumuiya ya Kimataifa kuwa
na siku maalum ya familia. Tanzania ikiwa ni mwanachama wa Umoja wa
Mataifa huungana na nchi nyingine kila mwaka kuadhimisha siku hii.
Post a Comment