Arusha. Baadhi ya mashabiki, wadau na wapenzi
wa soka jijini Arusha wamelalamikia hali ya uchafu wa vyoo vilivyopo
ndani ya uwanja wa michezo wa Kumbukumbu ya Sheikh Amri Abeid wakisema
vyoo hivyo mbali na kutoa harufu, lakini vinaweza kusababisha madhara
kiafya kwa binadamu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti juzi katika siku
ya wauguzi duniani iliyoadhimishwa kitaifa mkoani Arusha, baadhi ya
wakazi wa jiji hilo, walisema ni aibu kwa wamiliki wa uwanja huo ambao
ni Chama Cha Mapinduzi kushindwa kufanya usafi wa vyoo hivyo.
“Hii ni aibu kubwa kwa wamiliki wa uwanja huu,
ambao ni chama tawala, vyoo vinatoa harufu nzito, ni hatari kwa afya,”
walisema kwa nyakati tofauti
Diwani wa Kata ya Moshono, Paul Mathysen,
aliliambia gazeti hili kuwa alipata fursa ya kufika katika vyoo hivyo
juzi wakati wa sherehe hizo lakini kutokana na hali ya uchafu aliyoikuta
alishindwa kupata huduma.
Baadhi ya vibarua wanaofanya usafi ndani ya uwanja
huo walipohojiwa hawakutaka kuzungumzia suala hilo, lakini alipotafutwa
Katibu wa Uchumi na Fedha wa CCM mkoani Arusha, Hilal Sood, naye
alikwepa kutoa taarifa kwa gazeti hili pamoja na kutafutwa mara kwa
mara
Post a Comment