Dar es Salaam. Kamati ya maadili ya uchaguzi ya
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) bado haijatoa ripoti rasmi ya
wagombea ambao walienguliwa kwenye kinyang’anyiro cha uchaguzi huku
kukiwa na taarifa kuwa baadhi ya wagombea hawatarudishwa kwenye
kinyang’anyiro hicho.
Habari ambazo Mwananchi ilizipata
zinasema kuwa licha ya kamati ya maadili kuwasafisha, bado
haijawasilisha rasmi ripoti yake kwa maandishi, lakini TFF imekuwa
ikigomea kurejeshwa kwa wagombea hao.
“Kilichotokea ni kwamba kamati imewasafisha,
lakini haijawarejesha kwenye kinyang’anyiro, kusafishwa ni suala lingine
na kurudishwa ni suala lingine,” kilisema chanzo kimoja kutoka ndani ya
TFF na kuongeza:
“Suala kama la Rukambura, katiba ya TFF inaeleza
wazi mtu akienda mahakamani anaondolewa kujihusisha na masuala ya soka,
sasa kamati inamsafishishaje? haiwezekani wakarudishwa wote,
kinachosubiriwa ni huo uamuzi wa maandishi kutoka kamati ya maadili na
hatua nyingine zitafuatwa.”
Hivi karibuni wagombea saba walioenguliwa kwenye
kinyang’anyiro cha uchaguzi na kamati ya uchaguzi ya TFF iliyo chini ya
Hamidu Mbwezeleni kwa kile kilichoelezwa kuwa hawana hatia
walirudishwa.
Wagombea hao ni Kilungeja Nazarius, Riziki Juma, Wilfred Kidau, Shaffih Dauda, Omary Abdukadir na Richard Rukambura.
Post a Comment