Katika orodha ya wafungaji hadi sasa mshambuliaji
wa kimataifa wa Burundi na Simba, Amis Tambwe anaongoza akiwa
amezifumania nyavu mara sita katika mechi tatu alizoshuka di
mbani.
Mrundi huyo anafuatiwa kwa mbali na Chanongo
pamoja na washambuliaji wa Yanga, Didier Kavumbagu na Jerryson Tegete
ambao kila mmoja amefunga mabao matatu hadi sasa.
Hata hivyo,Tegete kwa muda mrefu sasa hayumo katika kikosi cha Stars kinachonolewa na kocha Kim Poulsen.
Mshambuliaji mwingine wa Stars aliyeingia katika orodha ya wafumania nyavu ni John
Bocco ambaye amefunga bao moja pekee.
Bocco anayetajwa kama mmoja wa washambuliaji bora
wa Tanzania msimu huu ameshindwa kuonyesha makali kutokana na
kusumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara. Mfungaji bora wa Ligi Kuu
msimu uliopia Kipre Tchetche wa Azam FC amefumania nyavu mara mbili.
Bocco ambaye amefunga bao moja pekee.
Post a Comment