Kitaalamu hufahamika kama empyema thoracis. Ni tatizo la kujaa
usaha katika chumba kinachotunza mapafu ndani ya kifua (pleural cavity).
Tatizo hili ni kubwa na lisipo tibiwa haraka, huleta madhara makubwa
ikiwa pamoja na kupoteza maisha. Hata hivyo, kupatikana kwa dawa za kuua
vijidudu (antibiotics) kumesaidia kupunguza vifo na madhara mengine
makubwa.
Tatizo hili husababishwa na magonjwa kadhaa ikiwa
pamoja na homa ya mapafu (nyumonia- Pneumonia), jipu la mapafu au
fangasi wa mapafu, Kifua Kikuu-TB, kuumia kifuani mfano kupata ajali au
kuchomwa na kitu kikali, maambukizi ini kwa juu.
Mgonjwa huwa na dalili za homa kali, mwili
kuchoka, kupoteza uzito, kukosa hamu ya kula, maumivu kifuani au mapafu,
kifua kupindia upande ulioathirika, kupumua kwa shida, kukohoa na kutoa
makohozi hutokea kama mgonjwa ana TB na Nyingine ni njia za hewa
kuunganika na chumba cha mapafu (bronchiopleural fistula) na jipu
kifuani ambalo huweza kutokea kutokana na usaha uliondani kujipenyeza
katikati ya mbavu. Jipu hilo huweza kupasuka, hivyo usaha mwingi
kuchuruzika nje.
Ni muhimu mgonjwa kwenda hospitali kufanyiwa
uchunguzi. Vipimo ambavyo huweza kufanyika na kubaini tatizo ni picha ya
kifua (X-ray), kutoboa kifua na kuuvuta usaha kwa sindano, kisha
kuupeleka maabara kwa uchunguzi, altrasound ya kifua ambayo husaidia
kubaini wingi wa usaha au kama usaha upo katika vijumba vidogodogo
(septated), CT scan huweza kusaidia iwapo tatizo limekaa zaidi ya siku
3, kwani huweza kuathiri mapafu na kifua vibaya zaidi, hivyo humsaidia
daktari katika uamuzi na kutoa matibabu sahihi.
Matibabu kwa tatizo hili ni kupitisha mrija
kifuani kutoa usaha kwa chombo maalumu, mgonjwa pia hupewa dawa kali za
kuua vijidudu, kama ana kifua kikuu basi dawa hutolewa pia. Kuzuia
tatizo lisijiruide, dawa au poda maalumu huingizwa katika chumba hicho
cha mapafu baada ya usaha wote kuwa umetoka (pleurodesis). Ikiwa mrija
umeshindwa kutoa usaha basi uhitajika upasuaji wa kutoa sehemu ya mbavu
moja kisha kupisha mrija mkubwa zaidi kutoa usaha. Iwapo mgonjwa amekaa
na tatizo hili kwa muda na mapafu yameathirika kwa kiwango kikubwa,
upasuaji mkubwa hufanyika kukwangua uchafu wote, kuharibu vijumba na
kutoa usaha kisha kusaidia mapafu kurudi walau katika hali ya kawaida.
Post a Comment