Mazoezi
Fanya mazoezi kwa kutembea mwendo wa haraka au
taratibu, kuendesha baiskeli au mazoezi y viungo. Wengi hunufaika kwa
kufanya mazoezi hayo kwani husaidia kutuliza fikra, kuimarisha misuli,
ukakamavu wa mwili na kumwezesha mtu kulala vizuri.
Hata ukifanya mazoezi hayo kwa dakika 20 pekee, utapata matokeo mazuri.
Hivyo ni vyema kutenga muda wako japo kidogo kila
siku, kufanya moja au zaidi ya mazoezi hayo ili kujiweka sawa kimwili na
kiakili.
Zingatia utaratibu mzuri wa kutunza kumbukumbu
Taarifa zote zinazohusu ugonjwa au magonjwa yanayomsumbua mtoto wako,
ziweke mahali pamoja. Taratibu za matibabu, tangu alipoanza kuugua;
vyeti au nyaraka nyingine zitunze zote mahali pamoja.
Namba za simu zote i muhimu kwako binafsi, familia
na kumbukumbu za masuala ya bima, vyote hivyo unatakiwa kuvihifadhi
mahali pamoja ambapo itakuwa rahisi kuvipata na kuvitumia
vinapohitajika.
Unapotafakari juu ya maswali ya kumuuliza daktari
akimtembelea mtoto wako, andika mara moja yanayofaa kwenye kijitabu
chako cha kumbukubu, kusudi usisahau kuomba taarifa unazohitaji pindi
atakapofika.
Omba msaada
Wanafamilia na rafiki zako wanaweza kuwa na shauku
ya kukusaidia, lakini wakawa hawana hakika ya namna unavyohitaji
kusaidiwa. Ikitokea wa kusema, “Kuna lolote ninaloweza kusaidia…,” na
ikawa lipo jambo unalohitaji kusaidiwa, unatakiwa kuwa wazi kwa
kumweleza hitaji lako bila kumung’unya maneno.Utashangazwa jinsi
shughuli hiyo itakavyofanywa kwa kasi, kutokana na utayari wa mhusika
uliochanganyika na kujitambua kuwa unamwamini, kiasi cha kumshirikisha
katika uhitaji wako.
Hali hiyo ya kueleza mahitaji yako kwa waliokaribu
na wewe siyo tu itasaidia kukuliwaza bali pia huyo anayekusaidia
atajisikia vizuri kwa kuwa miongoni mwa watu unaowaamini.
Tafuta msaada kwa makundi: Muulize daktari au
muuguzi wa mtoto wako, taarifa kuhusu makundi ya kijamii yanayosaidia
wenye matatizo yanayofanana na yanayomkabili mtoto wako.
Ikiwa unajisikia vizuri kumshirikisha mtu au watu
msiofahamiana sana matatizo yako, unaweza kufanya hivyo kwa kutumia
makundi mbalimbali, yaliyo katika mitandao ya kijamii.
Post a Comment