0
Dar es Salaam. Mshambuliaji wa Simba, Betram Mombeki amesema atahakikisha anaiongoza timu hiyo kutwaa ubingwa wa Lligi Kkuu msimu huu.
Mombeki ameendelea kuyafurahia maisha ndani ya klabu hiyo na kuonekana kuridhishwa na ufundi wa kocha wao, Abdallah Kibadeni.
A amesema hana wasiwasi na uchanga wa kikosi hicho na anaamaini bado Simba ina uwezo wa kunyakua ubingwa.
Akizungumza mara baada ya mchezo wao wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya SC Villa ya Uganda ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 4-1, huku Mombeki akifunga magoli mawili peke yake alisema chipukizi wa Simba wataiwashangaza mashabiki kwa soka safi watakalokuwa wakicheza.
“Sina shaka na kikosi chetu, ni kweli bado kichanga na wachezaji kama mnavyowaona wengi ni wageni, lakini hii haimaanishi tutashindwa kurudisha heshima ya Simba ya kutwaa ubingwa, nategemea ushirikiano wa wachezaji wenzangu na juhudi ziutatuweka katika nafasi nzuri zaidi,” alisema mshambuliaji huyo.
Katika hatua nyingine, Mombeki amewatahadharisha vinara wa ufungaji katika ligi hiyo na kudai lengo lake ni kuwa mfungaji bora wa ligi.
Simba inajiandaa na mchezo mwingine wa kirafiki utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa dhidi ya Three Pillars ya Nigeria.Subhead andika hapa , andika hapa,andika hapa Subhead andika hapa andika, andika hapa, subhead andika hapa, andika hapa,

Post a Comment

 
Top