TRA yakifunga kiwanda cha samaki
Musoma. Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imekifungia Kiwanda cha
Kusindika Minofu ya Samaki cha Prime Catch (Export) Ltd, baada ya
kushindwa kulipa mapato ya Sh1.1 bilioni. Akizungumza baada ya
kukifungia kiwanda hicho, Ofisa Kodi wa TRA kutoka Dar es Salaam, Toans
Silvanus alisema kiwanda hicho kimeshindwa kulipa deni hilo la mwaka
mmoja. “Kiwanda hiki kimekuwa kikikumbushwa kulipa mapato mara kwa mara,
barua wamekuwa wakiandikiwa kuhusu umuhimu wa kulipa mapato bila
shuruti, lakini wameshindwa,” alisema. (Florence Focus)
Post a Comment