Na Mwandishi Wetu
(email the author)
Dar es Salaam. Benki ya Exim Tanzania imeendelea kujiimarisha
kwa Sekta ya Benki baada ya kutajwa katika utafiti uliofanywa na Kampuni
ya Kimataifa ya Ukaguzi wa Hesabu ya KPMG, kuwa miongoni mwa benki
zinazowajali wateja nchini.
Kwa mujibu wa utafiti huo uliofanywa na KMPG kwa
Sekta ya benki kwenye nchi 14 barani Afrika, ulihusisha masuala
mbalimbali ya huduma kwa wateja.
Utafiti huo ulifanyika kati ya Juni na Desemba
mwaka jana, Benki ya Exim iliongoza kwa kujali wateja wake nchini
ikifuatiwa za Benki ya Barclays na Akiba Commercial (ACB).
“Benki ya Exim imeweza kupata alama 75.2 kwa jumla
kwenye suala la kumjali mteja, ikifuatiwa na Barclays alama 75 na Akiba
Commercial Bank (ACB) alama 74.9,” ripoti hiyo inasema.
Akizungumzia utafiti huo, Mkurugenzi Mtendaji wa
Benki ya Exim Tanzania, Anthony Grant alisema matokeo hayo ni changamoto
kwa benki yake na kwamba, wataongeza juhudi ili kupata mafanikio zaidi
miaka ijayo. “Huu ni mwaka mzuri kihistoria kwa benki yetu. Matokeo haya
ya utafiti yamekuja muda mfupi baada ya benki kuteuliwa katika Tuzo ya
Benki Bora barani Afrika mwaka huu,” alisema.
Post a Comment