Kwa ufupi
Alisema wakurugenzi na makatibu tawala wanatakiwa
kubeba dhamana kwa niaba ya Serikali na kuhakikisha wananchi wanapata
maendeleo yanayotakiwa.
SHARE THIS STORY
Morogoro. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Hawa
Ghasia amewaagiza makatibu tawala na wakurugenzi wa halmashauri nchini
kusimamia fedha za umma kwa uaminifu na kurejesha imani kwa wananchi na
Serikali na kusoma taarifa ya mapato na matumizi kila baada ya miezi
mitatu.
Ghasia aliyasema hayo mkoani Morogoro wakati
akifunga mafunzo ya siku nne ya wakurugenzi na makatibu tawala wote
nchini mkoani Morogoro.
Alisema wakurugenzi na makatibu tawala wanatakiwa
kubeba dhamana kwa niaba ya Serikali na kuhakikisha wananchi wanapata
maendeleo yanayotakiwa.
Alisema makatibu tawala na wakurugenzi kwa kila
mkoa wanatakiwa kuandaa utaratibu wa kutoa ajira kwa wanawake na vijana
wamachinga baada ya kutumia nguvu kuwaondoa katika maeneo yao ya
bihashara .
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu (Tamisemi), Jumanne Sagini alisema lengo la mkutano huo lilikuwa
kuwakumbusha washiriki husika malengo ya kazi na uzoefu wa kazi kwa
wakurugenzi wapya katika kusimamia rasilimali fedha na watu.
Alisema mkutano huo utawewezasha kubadilishana
uzoefu wa kazi ili waweze kufanya kazi kwa ushirikiano na kutimiza ahadi
walizopewa na wananchi
0inShare
Post a Comment