Morogoro. Baadhi ya wananchi wa mkoani Morogoro wametoa maoni
yao kuhusiana na rasimu ya Katiba Mpya ambayo ilizinduliwa Juni 3 mwaka
huu jijini Dar es Salaam na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dk Mohamed Gharib Bilal.
Wananchi hao ni pamoja na wanaharakati, wasomi wa
vyuo vikuu pamoja na watendaji wa mamlaka na idara mbalimbali za
Serikali wengi wao walionyeshwa kuridhishwa na rasimu hiyo.
Akizungumzia rasimu hiyo, Robert Selasela ambaye
ni msomi wa Chuo Kikuu Mzumbe alisema endapo rasimu hiyo itapitishwa
kipengere cha Spika na Naibu Spika kutotoka kwenye vyama kutaweza
kusaidia kuondoa malalamiko na malumbano yanayotokea bungeni.
Kwa upande wake Richard Kabate ambaye ni Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa alisema kuwa kuanzishwa kwa Mahakama
ya Juu kutaweza kupanua wigo wa utoaji na upatikanaji wa haki kwani
wananchi watakuwa na uwezo wa kukata rufaa katika mahakama tatu tofauti.
Naye Amani Mwaipaja ambaye ni mwanasheria wa
kujitegemea na mwanaharakati wa haki za binadamu alisema kuwa kuwekwa
kwa kiwango cha elimu kwa Spika, Naibu Spika na wagombea wa nafasi
nyingine kutasaidia kuondokana na tatizo la kuwa na viongozi wasio
wasomi ambao wamekuwa wakishindwa kuchambua mambo muhimu yanayohusu
nchi.
kwamba kutasaidia kuondokana na kero za Muungano ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kwa kipindi kirefu bila ufumbuzi.
Post a Comment