Katika Uwanja wa wazi mji wa E'el Ali iliyo katika mkoa wa Hiraan
katikati mwa Ardhi ya Somalia jana ilifanyika hukumu ya Haddi ya Jaldi
ambayo ilitekelezwa kwa mwanaume anaejulikana kwa jina la Bashir Ibrahim
Abdullahi aliyembaka mwanamke aliyekuwa na mtoto mchanga.
Mwanaume
huyo aliyeshtakiwa na Mlalamikaji ambae ndie aliyetendewa unyama huo
amekiri mbele ya Mahakama kuwa alifanya kitendo hicho huko akiwa na
akili yake timamu wakati akitenda kosa hilo,baada ya kusikiliza kesi
hiyo Mahakama ilitoa na kutangaza hukumu.
Bashir
alihukumiwa kulipa Mahari ya Mwanamama huyo,na kuhamishwa kutoka katika
mji huo kwa muda wa mwaka mmoja,kuchapwa viboko 100 mbele ya kadamnasi
waliohudhuria kushuhudia hukumu hiyo ikitekelezwa.
Katika
Mikoa ya Kiislaam nchini Somalia yalio chini ya Utawala wa Mujahidina
wanawake wa Kiislaam wamepata Heshima na Izza huko wakiwa huru kwenda
kokote watakao bila kubughudhiwa lakini maeneo yanayoshikiliwa na Maadui
wanawake wa Kiislaam hupata madhila na kuchezewa heshima na karama zao.
Post a Comment