Wanasiasa nchini Kenya kwa mara nyingine tena wameitaka Serikali ya
Uhuru Kenyatta kuwaondoa haraka wanajeshi wake waliopo nchini Somalia
ambapo walikivamia miaka minne iliyopita.
Waziri
mkuu wa zamani nchini Kenya Raila Odinga na ambae ni kiongozi wa Baraza
la wapinzani amesema akiwa mjini Mombasa kuwa usalama wa Kenya
utapitikana endapo wanajeshi wa Kenya waliopo nchini Somalia
wataondolewa haraka.
"Serikali
ya Kenya ni lazima iwaondoe wanajeshi walioko Somalia na kama hatua
hiyo haitachukuliwa mapema basi usalama wa ndani ya Kenya utaendelea
kuyumba na Al-Shabab wataendelea na mashambulio yao",alisema Odinga.
Ameilaumu
umoja wa Afrika kwa kuingiza Kenya vita ambayo ni ngumu na iliyogharimu
maisha ya mamia ya raia wa Kenya na kuiyumbisha uchumi wa nchi.
"Ili
kupunguza mashambulio yanayofanyika ndani ya Ardhi yetu ni vyema
utawala wa Kenya kuangalia suala hii kwa kuwaondoa wanajeshi wetu
walioko Somalia,ni kawaida kwa taifa yeyote kuchukua uamuzi mgumu wa
kuokoa maisha ya wananchi wake pamoja na nchi yake kwa ujumla",Odinga.
Mashirika
mbalimabli ya kiaria pamoja na vyama vya upinzani wanatoa shinikizo kwa
Uhuru Kenyatta kuwaondoa Wanajeshi wa Kenya walioko nchini Somalia
tangu kufanyika mashambulio ya mji wa Garissa yaliogharimu mamia ya
maisha ya wananchi wa Kenya.
Post a Comment