Habari kutoka mji wa Bosaso zinaeleza kuwa mapigano makali
yamefanyika usiku wa kuamkia leo karibu na majengo ya Ikulu ya Rais
katika utawala uliojiita wa Puntland kaskazini mashariki mwa Somalia.
Milio
ya risasi waliokuwa wakirushiana yalisikika katika eneo la kizuizi la
Ikulu ya mji wa Bosaso,walioshuhudia wanasema walisikia milio ya Risasi
na silaha ya kurushwa Begani.
Habari
za kuaminika zimethibitisha kuwa Kikosi kinachounga mkono Harakat
Al-Shabab Al Mujahideen walifanya mashambulio ya pembe tatu dhidi ya
wanamgambo waliokuwa wakilinda Majengo ya Ikulu.
Mpaka
sasa haijajulikana hasara iliyosababishwa na mashambulio hayo ya mji wa
Bosaso kutokana na kuwa usiku wenye giza nene na wanamgambo wa utawala
wa Puntland nao kufunga Barabara zote muhimu ya mji huo.
Post a Comment