Biashara ya Hawala.Baadhi ya mashirika ya kutoa misaada yameonya kwamba yatasitisha shughuli zao zote nchini Somalia iwapo Kenya itaendeleza marufuku ya biashara hiyo
Mashirika
ya kimataifa ya kutoa misaada ya kibinadam, yameonya kuwa huenda
yakalazimika kusitisha shughuli zao zote nchini Somalia, ikiwa Kenya
itabadili uamuzi wake wa kufunga vituo vya kutuma na kubadilisha sarafu
za kigeni maarufu kama hawala, kufuatia shambulio lililofanywa na
wapiganaji wa Al shabaab, katika chuo kimoja kikuu mjini Garissa.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa mashirika kumi na tano ya misaada,
mashirika hayo hutumia vituo hivyo kutuma pesa nchini Somalia na kulipa
mishahara na kodi kwa wafanyakazi wake.Mashirika hayo yamesema, agizo hilo litakuwa na athari kubwa sana kwa raia masikini wa Somalia, kwa sababu wao hutegemea fedha wanazopokea kupitia vituo hivyo kununua chakula, kulipa karo na pia kupata huduma za afya.
Serikali ya Kenya imesema imefunga vituo hivyo ili kuzuia kundi hilo la Al shabaab kupokea fedha kutoka kwa wafadhili wake katika mataifa ya kigeni.
Post a Comment