0

 
 Waziri wa masuala ya ndani nchini Afrika kusini ametoa wito kwa viongozi wa kitamaduni kukoma kutoa matamshi yasiyo na msingi ambayo yanaweza kusababisha maafa.
Waziri Malusi Gigaba amesema hayo baada ya mfalme wa Kizulu, Goodwill Zwelithini kusema kuwa wahamiaji wanapaswa kufunga virago vyao na kuondoka nchini humo.

 
Mfalem wa Afrika kusini Goodwill Zwelithini
Idara ya polisi nchini humo imesema kuwa zaidi ya wahamiaji elfu moja wameondoka kutoka mji wa mashariki mwa Durban katika kipindi cha siku chache zilizopita, kwa hofu ya kushambuliwa na raia wa nchi hiyo.
Raia wa kigeni hushambuliwa mara kwa mara nchini Afrika Kusini.



Post a Comment

 
Top