Serikali ya Kenya imetangaza kuwa iko tayari kufanya mazungumzo na
Harakat Al-Shabab Al Mujahideen inayoendesha harakati zake nchini
Somalia na ndani ya Ardhi ya Kenya.
Kiongozi
wa waliowengi katika Bunge la Kenya Adan Barre Duale amesema akiwa
katika mji wa Garisa kuwa Kenya inataabika na mashambulio ya mara kwa
mara kutoka kwa Harakat Al-Shabab Al Mujahideen na kwa hivyo basi hakuna
budi kufanya mazungumzo nao.
"Tuko tayari kufanya mazungumzo na Al-Shabab tutawatumia viongozi wa Kidini na watuambie tu mahali waliko",alisema Adan Barre.
Amesema
Jamii ya kisomali waliopo nchini Kenya hawakuwaradhi Uvamizi wa
wanajeshi wake kuingia nchini Somalia,Vikosi vya Harakat Al-Shabab Al
Mujahideen vimekuwa vikiendesha mashambulio ya mara kwa mara katika miji
mikubwa nchini Kenya.
Haifahamika
uwezekano wa kufanyika Mazungumzo kati ya Mujahidina wa Somalia na
Serikali ya Kenya ambao wanajeshi wake wapo katika uvamizi nchini
Somalia.
Post a Comment