Watu waliokuwa wamejihami na silaha wamemwua Afisa wa Serikali
shirikisho ya Somalia FG kwenye Wilaya ya Daniile mjini Mugadishu.
Walioshuhudia
wanasema watu waliokuwa na silaha za Pisto walimpiga risasi mkuu wa
Michezo katika Utawala wa Mungaabo Wilayani Dayniile,Afisa huyo
aliyeuawa alishawahi kulengwa mara kadhaa na kunusurika kwenye
mashambulio hayo yaliolenga kummaliza.
Upande
mwingine watu waliokuwa na silaha walimpiga risasi na kumwua papo hapa
mjini Marka Afisa mmoja wa kitengo cha Ujasusi wanaojulikana PS ambao
husaidiana na wavamizi wa Misalaba waliojiita AMISOM.
Katika
miezi ya hivi karibuni mauaji inayowalenga maofisaa wa Serikali
Shirikisho ya Somalia FG yameongezeka katika mji wa Mugadishu na mikoa
mengine nchini Somalia.
Post a Comment