0
Kwa miaka zaidi ya 25 ya muziki wake, Mariah Carey amekuwa miongoni mwa wanamuziki wanaovutia zaidi lakini hiyo haiji kirahisi.
Charmbracelet-photoshoot-mariah-carey-36859303-500-500
Kwa mujibu wa kesi iliyofunguliwa na mpiga picha mmoja dhidi yake, Mariah hutumia kiasi kikubwa cha fedha kujiandaa kwaajili ya photoshoot. Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa muimbaji huyo mwenye miaka 45 anahitaji kupambwa kwa gharama ya $85,000 (zaidi ya shilingi milioni 142) kabla hajaanza kupigwa picha.
mariah-3-mariah-carey-30459069-1024-768
Nyaraka hizo zinadai kuwa Mariah anahitaji huduma hiyo kutoka kwa stylist maarufu anayegharimu $65,391. Kisha kuna mtu anayemtengeneza nywele, $9,600 na make-up artist, $7,200. Kutengeneza kucha zake pia hugharimu $2,400.
Mpiga picha huyo aliamua kushtaki baada ya kujiandaa kwa photoshoot kwaajili ya kava la album yake ambayo ilisitishwa bila sababu. Anataka alipwe $150,000 za ada ya huduma hiyo.

Post a Comment

 
Top