Kwa mujibu wa Pulse Magazine la Kenya, Wizkid alikamatwa akivuta bangi ndani ya hoteli hiyo kitu ambacho hakiruhusiwi. Ofisa mmoja wa hoteli hiyo alimuuliza kwanini anavuta bangi ndani ya hoteli hiyo na hivyo wakajikuta wakiwakiana na walinzi kuingilia kati kabla ya polisi kuitwa na kumkamata.
kabla ya kupelewa kwenye kituo cha polisi cha Capital Hill ambako alihojiwa, hoteli hiyo ilimpiga faini ya shilingi 50,000 za Kenya ambazo alizilipa kwa credit card.
Victoria Kimani ndiye aliyemsaidia kumtoa kituoni hapo. Wizkid alitakiwa kuondoka saa tisa mchana siku hiyo lakini kutokana na drama hiyo aliahirisha safari.
Post a Comment