Senzo na mpenzi wake Kelly Khumalo
Mlinda mlango huyo wa Orlando Pirates aliuawa jana baada ya kupigwa risasi kifuani mbele ya mpenzi wake ambaye ni muimbaji na muigizaji. Katika tukio hilo, watu wawili waliivamia nyumba hiyo liyopo katika mji wa Vosloorus na kutaka wapewe simu, fedha na mali zingine.
Hii ni picha ambayo Kelly aliiweka kwenye akaunti yake ya Instagram, Jumapili, masaa kadhaa kabla ya Senzo (kushoto) kuuawa
“Senzo alitaka kumlinda Kelly sababu mmoja wao alikuwa amemwelekezea bunduki,” afisa mmoja aliwaambia waandishi wa habari. Polisi wanadai kuwa siku ya jana watu watu wawili waliingia nyumbani kwa Khumalo saa mbili usiku huku mwingine akisubiri nje na walipomaliza walikimbia.
Orlando Pirates, imeandika kwenye Twitter: “@Orlando-Pirates family has learned with sadness of the untimely death of our number 1 keeper & captain Senzo Meyiwa.”
Irvin Khoza, mwenyekiti wa club hiyo ameongeza: “This is a sad loss to Senzo’s family especially his children, to Orlando Pirates & the nation.”
Post a Comment