Kiungo huyo alikwenda kufanyiwa vipimo vya MRI katika goti lake na chama cha soka nchini Ujerumani ambacho kimethibitisha atakuwa nje kwa miezi mitatu. Kiungo huyo, 25, ambaye anaichezea Ujerumani, alicheza dakika 90 katika mechi ya Arsenal 0-2 Chelsea siku ya Jumapili.
Habari za kuumia kwake zinazokuja mwezi wa pili ndani ya msimu mpya, ni pigo kwa kocha Arsene Wenger ambaye sasa idadi ya majeruhi inaongezeka katika timu yake. Ozil akiungana na Aaron Ramsey, Mathieu Debuchy, Olivier Giroud pamoja na Mikel Arteta.
Post a Comment