Wawili hao walikuwa nchini Kenya mwezi uliopita kurekodi kipindi Coke Studio Africa msimu wa pili.
“Tulimkabidhi Diamond cheque ya fedha nyingi za mirahaba na baada ya kumuonesha michakato yetu, alikuwa tayari kusaini nasi,” alisema CEO wa MCSK, Maurice Okoth.
“Kwa sasa Diamond ndiye msanii wa nje maarufu zaidi na msanii wa nje aliyepata fedha nyingi za mirahaba. Yemi alikuwepo pembeni wakati tunamuonesha Diamond hatua za kusaini na yeye akafurahishwa sana na ofa yetu na hapo ndipo tulimsainisha pia.”
Maurice alidai kuwa tuzo za MCSK zitafanyika October 20 kwenye hoteli ya Safari Park jijini Nairobi ambapo Diamond, Jose Chameleone, Eric Wainaina, M.O.G Bahati, P-Unit, Size 8 na Bahati ni miongoni mwa wasanii watakaohudhuria.
Chanzo: The Star Kenya
Post a Comment