Muimbaji wa R&B anayetamba kwa sasa, August Alsina alijikuta
akipata vifafa vya hapa na pale baada ya kuanguka wakati akitumbuiza
jukwaani saa 24 zilizopita. Bado ameendelea kulazwa hospitali.
Mwakilishi wa msanii huyo ameuambia mtandao wa TMZ kuwa msanii huyo
amelazwa kwenye wodi ya wagonjwa mahututi jijini New York na anapewa
matibabu ya kifafa. Alsina alizimia na kuanguka wakati akitumbuiza usiku
wa jana jijini humo.
Amesema madaktari hawakukuta dawa zozote kwenye mwili wake zaidi ya
bangi kwenye mfumo wake. Wanaamini kuzimia kwake kulitokana na kuchoka
na kukosa maji.
Post a Comment