Ijumaa iliyopita, Nicki Minaj aliandika malalamiko yake
kwenye akaunti yake ya Twittter akidai kuwa mkuu mpya wa shule aliyosoma
alimzuia kuingia shuleni hapo kuongea na wanafunzi kwa lengo la
kuwainspire.
Wengi walidhani kuwa tatizo ni video na picha zisizo na maadili za
Nicki Minaj ambazo zilimfanya mwalimu huyo kudhani asingekuwa mfano
mzuri kwa wanafunzi wake.
Lakini kwa mujibu wa Mediatakeout, moja kati ya wajumbe wa baraza la wazazi waliweka wazi sababu ya Nicki kunyimwa kibali.
Ameeleza kuwa Nicki Minaj alilenga katika kutaka kujitangaza zaidi
kwa kuwa baada ya kukatazwa na kitengo cha elimu cha New York kuingia
na wapiga picha za video kwenye shule hiyo.
“Ukweli ni kwamba Ms. Minaj aliambiwa na kitengo cha elimu cha New
York (NYC Department of Education) kuwa asingeruhusiwa kuingia shuleni
pale na crew ya television. Kitengo hicho kina sera zake kulinda faragha
na usalama wa kila mwanafunzi. Nina uhakika wote tunakubali
utekelezwaji makini wa sera hii kwa kuzingatia usalama wa watoto wetu.
Ameongeza kuwa Nicki Minaj alitaka kuweka kwenye video kila
kitakachofanyika pale kama sehemu ya kampeni ya kujitangaza kwa umma kwa
mazuri anayofanya.
“If it’s a PR war Miss Nicki wants, she’s going to lose. What if
she had just played by the DOE’s guidelines? That would have been too
easy.
Post a Comment