Mshambuliaji wa klabu ya Barcelona ya nchini Hispania,
Neymar da Silva Santos Júnior ameteuliwa kuwa nahodha mpya wa kikosi cha
timu ya taifa ya Brazil ambayo hii leo itakabiliwa na mchezo wa
kimataifa wa kirafiki dhidi ya Colombia.
Kuteuliwa kwa mshambuliaji huyo ambaye alishindwa kumaliza kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 2014 kufuatia jeraha ya kiuno, kumetokana na mabadiliko yaliyofanywa na kocha mpya Carlos Dunga kwa kumpokonya kitambaa cha unahodha beki wa klabu bingwa nchini Ufaransa PSG, Thiago Silva.
Hatua hiyo itakuwa ni ya kwanza kwa Neymar mwenye umri wa miaka 22, kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Brazil, kama nahodha tangu alipoanza kukitumikia mwaka 2010.
Hata hivyo imeelezwa kwamba kuteuliwa kwa Naymar kuwa nahodha wa kikosi cha Brazil, kumechangiwa na kutokuwepo kwa beki Thiago Silva pamoja na aliyekuwa nahodha msaidizi David Luiz.
"Nahakika ana uwezo mkubwa wa kuwaongoza wenzake uwanjani na anakidhi kwa vigezo vyote, hivyo kumteua Neymar ninajua ninachokifanya kwa kusudio la kukisuka upya kikosi cha Brazil," Dunga aliwaambia waandidhi wa habari
"Ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu, licha ya kuwa na umri mdogo lakini ninaamini anaweza kukamilisha majukumu yake uwanjani pamoja na kuwaelekeza wengine kile nitakachowaagiza kufanya.” Ameongeza Dunga
Kikosi Cha Brazil kuitarejea uwanjani hii leo huku kikiwa na kumbu kumbu mbaya katika michezo yake miwili ya mwisho wakati wa fainali za kombe la dunia ambapo kama inakumbukwa vyema wenyeji hao wa fainali hizo walikubali kufungwa mabao matatu kwa sifuri dhidi ya Uholanzi na kabla ya hapo walikubali kufungwa mabao saba kwa moja dhidi ya Ujerumani.

Post a Comment